Ulipitwa na matokeo ya michuano ya ligi ya Europa? Nimekusogezea hapa
Kwa upande wa timu ya AS Roma imejikuta ikiangukia pua baada ya kufungwa goli 3-0 nyumbani baada ya kucheza na Fiorentina, timu zote kutoka nchini Italy, kwa matokeo hayo Roma imetupwa nje kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wao awali.
Nayo Inter Milan ikakwaa kisiki baada kufungwa goli 2-1 dhidi ya Wolfsburg ya Ujeruman na kutolewa kwenye mashindano hayo kwa magoli 5-2 baada ya awali kufungwa mabao 3-1, huku Villarreal ikichapwa goli 1-2 dhidi ya Sevilla na kutolewa nje kwa goli 5-2 ambapo mechi ya kwanza walifungwa goli 3-1.
Mashindano hayo ya Europa kwa sasa yanaingia katika hatua ya robo fainali.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment