Tangakumekuchablog
Tanga, MKUU wa
Majeshini nchini, Devid Mamunyange, ameliagiza jeshi la polisi na vikosi vya
Usalama Tanga kuhakikisha majambazi waliofanya mauaji ya kutisha kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga wanakamatwa haraka.
Ameyasema hayo jana wakati wa mazishi ya watu 8 waliouwawa
kwa kuchinjwa usiku wa Jumatatu na kusema kuwa msako wa kuwatafuta watu hao ufanyike
mara moja.
Amewahakikishia wananchi wa Amboni
na Tanga kwa ujumla kuwa Jeshi la Wananchi na vyombo vyengine vya Usalama
likiwemo Polisi kuwa tukio kama hilo haliwezi tena kujirudia.
Kwa wake Inspector Jenerali wa Polisi nchini , Enerest
Magu, amewataka polisi kuzidisha ulinzi wa watu na mali zao usiku na mchana ili
kuondosha hofu kwa wananchi juu ya usalama wao.
Amesema kufuatia tukio hilo wananchi
wameingiwa na hofu na kazi za kujiletea maendeleo kudorora ikiwemo kilimo na mifugo hivyo kuwataka
kuongeza doria maradufu.
Usiku wa kuamkia juzi watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliwauwa
watu 8 kwa kuwakusanya kwa pamoja na
kuwachinja mmoja mmoja mbele ya uwanja
wa nyumba ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji tukio ambalo limewashangaza
watu wengi.
Mwisho
Makamanda wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ngazi mbalimbali wakishiriki mazishi ya watu 8 waliochinjwa na watu wanaoaminika kuwa ni majambazi kitongoji cha Kibatini kayta ya Mzizima Amboni Tanga na mazishi yake kufanyika jana.
Umati wa watu wa Kibatini, Amboni na Tanga wakishiriki katika mazishi ya watu 8 waliuwawa kwa kuchinjwa na watu wanaoaminika kuwa ni majambazi usiku wa Jumatatu
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment