UNDANI WA KIFO CHA KEPTENI JOHN KOMBA!
Marehemu Kapteni Komba.
HabariKwa hisani ya http://www.globalpublishers.info/
Picha ya kwanza ya Marehemu komba mara baada ya kufariki dunia.
…Komba enzi za uhai wake.
MBUNGE wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba amefariki dunia jioni hii jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.
Mmoja
wa watoto wa Komba ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Herman
amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, huku akilia, msiba wa
baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar.
Habari
zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi
kama kawaida lakini baadaye akajisikia vibaya, hivyo akaamua kurudi
nyumbani ambako alizidiwa ndipo familia yake ilipoamua kumkimbiza
Hospitali ya TMJ lakini alipopimwa na madaktari ikathibitika kuwa
alikuwa tayari ameaga dunia. habari zaidi zinasema kuwa hivi sasa mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Kapteni
Komba ambaye pia ni Mkurugugenzi wa Kikundi cha Maigizo cha Tanzania
One Theatre (TOT), ambacho kina kikundi cha taarabu na bendi
inayokwenda na mtindo wa Achimenengule, amekuwa akikisaidia sana chama
chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni zake wakati wa uchaguzi
kwa kutunga nyimbo za kuhamasisha wapiga kura na kushiriki kupiga live
kwenye majukwaa ya kisiasa.
…alipokuwa bungeni
Enzi
za uhai wake alitamani sana na kufanya juhudi kubwa ili mtindo wa
Achimenengule uwe wa kitaifa lakini ikashindikana, na badala yake
Watanzania sasa tuna muziki wa Mduara ambao umekuwa kama mtindo wa
muziki wetu kwa sababu zifuatazo.
Kwanza,
ni mtindo halisi wa Kitanzania uliochipuka kutoka mahadhi ya kimwambao
ya Tanzania. Pili, ndiyo mtindo pekee uliowahi kutumiwa na bendi nyingi
baada ya kuasisiwa na ‘mabingwa’ wa muziki wetu, wana Njenje, The
Kilimanjaro Band.
Baada
ya bendi hiyo kuuasisi, mtindo huo, tayari umepigwa na bendi kama TOT
Plus, Chuchu Sound, Pamo Sound, Inafrika Band, wana mipasho kadhaa na
mwanamuziki mahiri lakini asiyethamini kiwango chake kikubwa cha muziki,
Bob Haisa.
Sababu
ya tatu ni kwamba mtindo huo umekuwa wa kupigwa na bendi nyingi,
vikundi vingi na wanamuziki wengi si kwa kulazimisha bali kwa mapenzi tu
ya mashabiki wa muziki wa Tanzania.
Kapteni
Komba awali alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuingia jeshini
na kuwa kiongozi wa kikundi cha maonesho cha jeshi na baadaye Rais
Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akamshawishi aachane na jeshi na kujiunga na
CCM wakati wa mfumo wa vyama mingi ulipoingizwa mwaka 1992.
“Mzee
Mwinyi ndiye aliyenifanya niache jeshi wakati huo nikiwa na cheo cha
ukapteni. Aliniomba nikisaidie chama kwa kuanzisha kikundi ambacho lengo
lake lilikuwa kukipigia debe CCM,” aliwahi kusema hivyo Kapteni Komba.
Ameshiriki
kampenzi za marais Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na aliye
madarakani hivi sasa, Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi hadi
kifo kinamchukua.
Licha ya siasa Kapteni Komba alikuwa anamiliki shule na pia alikuwa na biashara kadhaa.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.
Baada
ya kurejea nchini alisema upasuaji huo ulichukua saa tano na ulifanyika
katika Hospitali ya Apollo, India na alikanusha kuwa alikuwa na ugonjwa
wa figo.Ugonjwa uliomuua ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa
likimsumbua kwa muda mrefu.
..marehemu
Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake Mbezi tangi Bovu akielezea
kuimarika kwa afya yake aliporejea kutoka India kwenye matibabu, Julai
27, 2012.
Marehemu Komba ameacha mjane,
Bi Salome, ambaye ni mwalimu kitaalumu na watoto kadhaa. Mungu ailaze
roho ya marehemu mahali pema peponi- ameen!