Kutoka MAGAZETI ya leo Tanzania February 26, 2015 hapa nimekuwekea STORI 8 zilizopewa Headlines…
MWANANCHI
Kundi la Wanamgambo wa kiislamu la Al Shabaab lenye makao makuu yake Somalia limetishia kuzishambulia nchi za Magharibi ikiwemo Marekani.
Kundi hilo limesema kuwa litashambulia maeneo ya mbalimbali ya kibiashara yaliyopo katika nchi hizo.
Kupitia mtandao wa Twitter kundi hilo limesema litashambulia maeneo ya Mall of America mjini Minnepolis nchini Marekani, Forum des Halles mjini Paris nchini Ufansa.
Al Shabaab walisema kuwa zitashuhudia
mashambulizi yanayofanana na yaliyotokea Nairobi nchini Kenya mwaka 2013
ambapo watu 60 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa.
Waziri wa Usalama wa Marekani Jeh Johnson aliwataka
raia wa nchi hiyo kuwa makini katika kutoa taarifa kwa vyombo vya
usalama ili kudhibiti mashambulizi ambayo yanweza kutokea.
MWANANCHI
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge
ameibuliwa tuhuma nzito kwenye Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma baada ya kudaiwa kuwa aliishawishi kampuni ya
Independent Power Solution Limited (IPTL)
kuingia mkataba na Tanesco na baadaye kuwa mshauri wa kampuni hiyo
binafsi iliyomuingizia Sh1.6 bilioni zinazohusishwa na sakata la Akaunti
ya Tegeta Escrow.
Hata hivyo, Chenge, ambaye ni mhitimu wa Shahada ya Umahiri wa Sheria kwenye Chuo Kikuu cha Harvard
cha Marekani, aliwasilisha amri ya zuio ya Mahakama Kuu inayokataza
chombo chochote cha Serikali kujadili sakata la escrow hadi hapo shauri
lililopo mahakamani litakapotolewa uamuzi, jambo lililozua mjadala wa
kisheria na kusababisha mwenyekiti wa Baraza la Sekretarieti ya Maadili,
Jaji Hamisi Msumi, kuahirisha hadi leo.
Chenge ni mmoja wa watu kadhaa
wanaotarajiwa kuhojiwa na kamati hiyo kutokana na kuhusishwa na kashfa
ya uchotwaji wa zaidi ya Sh306 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta
Escrow iliyofunguliwa Benki Kuu kwa makubaliano kati ya Tanesco na IPTL baada ya pande hizo mbili kutofautiana kuhusu tozo za malipo ya umeme unaozalishwa na kampuni hiyo binafsi.
Mwingine ni mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Anna Tibaijuka,
aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ambaye pia
aliingiziwa kwenye akaunti yake Sh1.6 bilioni zinazohusishwa na akaunti
hiyo ya escrow.
Wote wawili waliingiziwa fedha hizo na
James Rugemarila, mkurugenzi wa VIP Engineering iliyokuwa ikimiliki
asilimia 30 ya hisa za kampuni ya IPTL.
Lakini jana, akisoma hati ya malalamiko
dhidi ya mbunge huyo wa Bariadi, mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili,
Hassan Mayunga alisema mlalamikiwa, akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG) mwaka 1995, aliishauri Serikali kuingia mkataba wa miaka 20 na IPTL
wa kuongeza uzalishaji wa umme.
“Mlalamikiwa
baada ya kustaafu wadhifa wa AG, Desemba 24 mwaka 2005, mwaka 2006
aliingia mkataba wa kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni ya VIP Engineering
and Marketing Limited iliyokuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa za IPTL,” alisema Mayunga akikariri hati hiyo ya malalamiko.
MWANANCHI
Utafiti mpya umebaini kuwa asilimia
kubwa ya Watanzania hawaridhishi na uwepo wa raia wa China nchini
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupokwa ajira.
Kadhalika utafiti huo uliofanywa na Afrobarometer kuhusu
uwepo wa raia wa China nchini una faida au hasara kwa Watanzania’
ulibaini kuwa licha ya kuzinunua wa wingi bidhaa za nchi hizo lakini
hawaridhishwi nazo.
Mtafiti kutoka Taasisi ya REPOA Stephen Mwambole
alisema wananchi 2,386 wa bara na visiwani walihojiwa kati ya Agosti 26
na September 29, 2014, kati yao 37% alisema bidhaa kutoka China zisizo
na ubora zinachafua taswira ya nchi hiyo,20% walisema Wachina waishio
nchini wamechukua ajira ambazo zingeweza kufanywa na Watanzania wenyewe.
“Watanzania wanafurahishwa na bidhaa za kichina lakini hawafurahishwi na ubora wake:-Mwambole.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa 81% ya
wasomi,72% wazee,wakazi wa mijini 77% na wanaume 75% ndiyo wanaofurahia
uhusiano uliopo kati ya nchi hizo.
HABARILEO
Mtoto Pendo Emmanuel
(4) mwenye ulemavu wa ngozi, aliyetekwa na kuchukuliwa na watu
wasiojulikana nyumbani kwao wilayani Kwimba, imegundulika alihifadhiwa
katika hoteli moja ya kifahari jijini Mwanza, kabla ya kukabidhiwa kwa
watu wengine, walioondoka naye kusikojulikana.
Imeelezwa kwamba mtoto huyo alikuwa
akilishwa chakula na watumishi wa hoteli hiyo, kabla ya kuchukuliwa na
kukabidhiwa kwa watu hao wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema mjini hapa jana kwamba Polisi inasaka watu hao waliokabidhiwa huku mzazi (baba yake), Emmanuel Shilinde, watumishi na mmiliki wa hoteli hiyo (haikutajwa jina) wakiendelea kuhojiwa.
Mulongo alitoa taarifa hiyo wakati wa hafla ya kuapisha wakuu wa wilaya wateule watatu, Pili Bayo wa Wilaya ya Kwimba, Zainabu Telaki wa Sengerema na Mwajuma Nyiruka wa Wilaya ya Misungwi.
Pendo alitekwa na watu wasiojulikana
usiku wa Desemba 27 mwaka jana nyumbani kwao katika kijiji cha Ndami
wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza baada ya watu hao kumpora akiwa amelala
na wazazi wake.
Baada ya kutoweka na polisi kutoa picha,
kuwezesha atakayemwona, kutoa taarifa, pia ilitangaza kutoa dau la Sh
milioni tatu kwa mtu atakayetoa taarifa, zitakazosaidia kupatikana kwa
mtoto huyo.
, “Baadaye
Pendo alichukuliwa na kukabidhiwa kwa watu wengine, ambao walitoweka
naye, kwa sasa serikali inawasaka watu hao waliokabidhiwa pale
hotelini.” Aliongeza, “Watu wote
waliokuwa wanamhudumia Pendo, mzazi wake na mmiliki wa hoteli ile
tunawashikilia ili watueleze alikopelekwa Pendo ingawa hatujui kama yuko
hai au amekufa.”
NIPASHE
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema hauna imani na uandikishaji wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa Biometric Voters Registration (BVR), kutokana na kugubikwa na kasoro nyingi katika siku za mwanzo za uandikishaji huo unaoendelea mjini Makambako, mkoani Njombe.
Pia umesema serikali haina sababu ya
kuwekeza fedha na muda kwenye kupiga kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa, kwani uandikishaji wa wapigakura kwa ajili ya uchaguzi
mkuu wa mwaka huu unasuasua.
Badala yake, umeishauri serikali kutumia fedha hizo kutoa elimu na kuhamasisha Watanzania kujiandikisha kwenye daftari hilo.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Prof. Ibrahim Lipumba, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inadanganya umma kuwa uandikishaji unaendelea vyema, wakati changamoto zilizojitokeza ni nyingi.
Alitaja kasoro zilizojitokeza kuwa ni
alama za vidole sugu kutokusomeka kwenye mashine za BVR, mashine kubagua
baadhi ya rangi za nguo na wafanyakazi kuchelewesha kazi hiyo kutokana
na kukosa uelewa wa matumizi sahihi wa mashine hizo.
“Serikali
kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), chini ya Mwenyekiti wake, Jaji
mstaafu, Damian Lubuva, waache kutudang’anya Watanzania kwamba zoezi
linaenda vizuri na kutuaminisha kuwa litakamilika ifikapo Aprili 16,
wakati kuna changamoto lukuki, ikiwamo kubwa ya ukosefu wa fedha,”:- Prof. Lipumba.
Aliitaka Nec kuweka hadharani ripoti ya
mshauri mwelekezi, Darall, kwa ajili ya Watanzania kuisoma na kujua
mfumo mzima unavyoweza kufanya kazi.
Alisema hakuna haja ya Rais Jakaya
Kikwete kutaka kukamilisha kazi ya upigaji kura ya maoni kwenye daftari
hilo wakati Watanzania hawajaandikishwa na wala serikali haina uwezo wa
kumaliza kazi hiyo kwa wakati na kwamba, haina fedha za kuendeshea.
NIPASHE
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika ‘kuiba’ mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Pendo Emmanuel (4), katika Kijiji cha Ndami, Wilaya ya Kwimba, mkoani humo wamekamatwa.
Akizungumza wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya wa mkoa huo jana, Manju Msambya (Misungwi), Zainab Rajab (Sengerema) na Pili Moshi (Kwimba), Mulongo alisema watu wote waliohusika wamekamatwa na hivi sasa bado hawafahamu kama mtoto huyo yupo hai ama mfu.
“Wezi
wale baada ya kumuiba mtoto Pendo walimleta katika hoteli moja hapa
jijini Mwanza, kisha kuwakabidhi watu walioonekana wanunuzi, lakini wote
hao wamekamatwa akiwamo mmiliki wa hoteli hiyo,” Mulongo.
Alisema serikali ipo kazini wakati wote,
ndiyo maana inafanya kazi usiku na mchana kuwasaka watu wote waovu
mkoani Mwanza ambao hawawezi kusalimika kwa kile watakachokifanya.
Hata hivyo, alisema watu hao waliofanya
uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa
na polisi huku mtu wa mwisho aliyetoweka na mtoto huyo toka hotelini
hapo akiendelea kutafutwa.
NIPASHE
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ilola, Kata ya Ilola Itwangi,
Wilaya ya Shinyanga Vijijini, mkoani hapa, mwenye umri umri wa miaka 12
(jina lake linahifadhiwa kutokana na umri wake), anashikiliwa na polisi
kwa tuhuma za kumuua mwenzake kwa kumpiga ngumi kichwani na kuangukia
kisogo, wakati wakigombea daftari waliloazima.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Longinus Tibishubwamu,
jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 7:30 mchana na kwamba,
wanamshikilia mwanafunzi huyo kwa mahojiano na kwamba wakikamilisha
upelelezi atafikishwa mahakamani.
Alimtaja mwanafunzi aliyefariki dunia kuwa ni Veronica Venance (12), aliyekuwa anasoma darasa moja na mwezake aliyesababisha kifo hicho.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Magere Jonas, alisema wakati wanafunzi hao wanagombea daftari hilo, alikuwa amepumzika chini ya mti akiwa na mwalimu mkuu msaidizi.
Jonas alisema baada ya kuingia darasani,
walimkuta mwanafunzi huyo akiwa amelala chini akigalagala, hivyo
kumkimbiza kwenye kituo cha afya Bugisi kilichoko jirani na shule hiyo,
lakini kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo alifariki dunia.
Mtendaji wa Kata ya Ilola, Mahona Joseph,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza marehemu alikuwa
ameng’anga’nia daftari alilokuwa ameazimwa na Sophia Mathew kwa ajili ya
kuandika ‘notes’ kitendo ambacho kilimkera mwenzake na kuzua ugomvi.
“Tunahisi
kifo cha mwanafunzi huyu kilitokana na kuanguka vibaya mara baada ya
kusukumiwa ngumi na kukipiga kisogo, hivyo kukata mawasiliano na
kusababisha kifo chake. Masuala mengi tumeviachia vyombo vya sheria”;-Joseph
MTANZANIA
Viongozi wa dini wameshauri majangali
watakaokamatwa na kuthibitika kufanya ujangili , wang’olewe meno ili
wasikie uchungu wa kufanya vitendo hivyo kwa wanyama.
Aidha alionya ni wakati kwa waovu hao
kufika mwisho na kuacha ujangili wa kuua wanyama na kuchezea rasilimali
nyingine za nchi bila kuchukua hatua.
Baddhi ya viongozi hao wadini walionya
kulegalega kwa viongozi wa Serikali na kushindwa kukabiliana na ujangili
na kwamba hali hiyo ni kuwadanganya wananchi katika jambo kubwa
linalohusu uchumi wao.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Alhad Musa Salum alisema umefika wakati wa viongozi wa dini kujitokeza
waziwazi na kuisaidia Serikali katika vita dhidi ya ujangili.
Askofu Joseph Mwingira alisema Serikali
ina dhamana ya kulinda rasilimali kama itasimamiwa vizuri ujangili
utaisha na umaskini nao utaisha.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment