Tangakumekuchablog
Tanga, NAIBU Meya halmashauri ya jiji la
Tanga, Muzzamilu Shemdoe amezitaka kamati za mazingira jijini humo kuhakikisha
zinafanya kazi zake na kusema kuwa kata yoyote ambayo itakuwa na mazingira
machafu viongozi wake watajibishwa.
Akizungumza
katika kongamano la mazingira lililowashirikisha wenyeviti wa Seikali za mitaa
na kata na kuandaliwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Nguvumali Community Development
Emviroment (NCDE) jana, Shemdoe alisema jiji la Tanga bado ni chafu.
Alisema
hali ya jiji hilo haliridhishi na hivyo
kuhitajika nguvu za ziada ikiwa na pamoja na elimu kwa wananchi na kutoa agizo
kwa kamati za mazingira kila kata kuhakikisha
maeneo yao yanakuwa safi muda wote.
“Ili
kuhakikisha kata zetu zinakuwa katika mazingira ya usafi ni lazima tujiwekee
sheria ndogondogo ambazo zitatusukuma jiji letu kuwa safi kama yalivyo majiji
mengine” alisema Shemdoe na kuongeza
“Kata
yoyote ambayo haitokuwa tayari kuonyesha dhamira ya kweli katika kuyaweka
maeneo yao safi tumejiwekea sheria ambazo viongozi wake tutawaita na
kujieleza sababu na wapi wamekwama”
alisema
Alizitaka
kamati hizo kufanya kazi zake na kuwa karibu na wananchi ikiwa na pamoja na kuhamasisha
wananchi kujua wajibu wao katika kuyaweka mazingira ya usafi sehemu zinazowazunguka.
Akizungumza
katika kongamano hilo, Katibu wa Asasi ya Nguvumali Community Emveroment
(NCDE), Frank Mgunda, alisema changamoto
inayowakabili wananchi ni vitendea kazi na kuwa chanzo cha jiji la Tanga kuwa
katika mazingira machafu.
Alisema
kutokuwa na vitendea kazi ni moja ya sababu ya mazingira hayo kuwa machafu na
kusababisha kwa baadhi ya mitaa kuzuka magonjwa ya miripuko nyakati za mvua
baada ya mitaro kujaa maji na kuzalisha mazalia ya mbu.
“Changamoto
kubwa ni uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi na utakuta viongozi wanahimiza usafi
lakini ukiangali kwa vifaa vipi-----kuna kuzibua mitaro na uzoaji wa taka ngumu
vyote ni vifaa” alisema Mgunda
Alisema
ili kuweza kufikia malengo ni vyema halmashauri kugawa vifaa vya kufanyia usafi
kila kata na kuweka mikakati ya eneo ambalo litaongoza kwa usafi kila mwezi
kupewa zawadi ili kuleta hamasa zaidi.
Alisema
kufanya hivyo kutasaidia kwa kiwango kikubwa kuwafanya wananchi kujua wajibu
wao wa usafi katika mazingira inayowazunguka
na hivyo kulitaka jambo hilo kulifanya mara moja.
Mwisho
No comments:
Post a Comment