Zimekupita Habari MAGAZETINI leo FEB21? Hapa ziko stori kubwa tano..
MTANZANIA
Kiongozi wa vijana waliopata mafunzo ya
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), waliokuwa wakiishinikiza Serikali
kuwapatia ajira, George Mgoba amelazwa katika Hospitali ya Amana Dar es
Salaam baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana tukio ambalo
linafanana na kile alichofanyiwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari, Dk.
Steven Ulimboka au Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd,
Absalom Kibanda.
Mgoba ni miongoni mwa vijana
waliowawakilisha wenzao zaidi ya 300 kukutana na viongozi wa juu wa
Serikali hivi karibuni, akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Sefue kuzungumzia kilio chao na kupinga upendeleo wa ajira ndani ya
Jeshi.
Gazeti la MTANZANIA lilifika Hospitalini
ambako lilifanikiwa kuzungumza na Msemaji wa vijana hao, Omary Bakari,
ambaye alisema alipokea simu saa nne siku ya Jumatatu hiyo hiyo
ikimtaarifu kuwa Mwenyekiti wao, Mgoba, amelazwa katika Hospitali ya
Tumbi, Kibaha ikimtaarifu kuwa mwenzao huyo alikuwa mahututi hospitali
hapo.
Alipozungumza na mgonjwa ili kufahamu
kilichompata alieleza kuwa alipigiwa simu na watu waliojitambulisha kuwa
ni vijana wenzake wa JKT
wakimtaka waonane eneo la Mabibo Mwisho ili wazungumze mipango ya maandamano.
wakimtaka waonane eneo la Mabibo Mwisho ili wazungumze mipango ya maandamano.
“Nusu saa baada ya kupigiwa simu alifika
eneo walilopanga na kukutana na watu hao ambao walikuwa ni wanawake
wawili na mwanaume mmoja, waliokuwa na gari aina ya Noah,” alisema.
Akinukuu maelezo ya mgonjwa, Bakari
alisema baada ya kusalimiana kwa kupeana mikono na wanawake hao, mmoja
wao alimwambia ajitoe kitu katika sikio na mara baada ya kufanya kitendo
hicho alihisi mwili kupata ganzi na hivyo kupoteza fahamu papo hapo.
Alisema baada ya kuhakikisha amezimia
inavyoonekana watu hao walimfunga kamba mikononi na miguuni na kisha
kitambaa usoni na kwenda naye kusikojulikana.
“Baada ya muda mchache kupita Mgoba
alipata fahamu na kujikuta akiwa amefungwa kamba pamoja na kitambaa
usoni na hakujua anakopelekwa, ila alisema wakati huo alihisi wanaingia
kwenye bonde ambako walimshusha,” alisema.
Alisema walipomshusha walianza kwa kumpiga, huku wakimtaka ataje ni nani aliyemtuma kuandamana kati ya Ukawa au Lowassa?
“Aliposhindwa kusema aliyemtuma ndipo
walipombana sehemu za siri, vidole na mbavu na kisha kumpiga mateke na
baada ya kumuona ameishiwa nguvu wakamvua nguo na kumlazimisha afanye
tendo la ndoa na mmoja wa wanawake hao,” alisema.
Alisema walipoona ameshindwa kufanya
tendo hilo wakamnyoa nywele na kisha kuanza kutafuta mshipa uliopo
pembeni ya paji la uso, lakini walishindwa kuupata na hivyo kuamua
kumchoma sindano mkononi.
“Walihakikisha hana nguvu, ndipo
walisikika wakisema wamemaliza kazi, hivyo wakamchukua na kumtupa msitu
wa Mailimoja wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
“Akiwa msituni alijisikia kupata fahamu, ambapo alianza kutambaa kuelekea barabarani ambako msamaria mwema mmoja alimuona na kisha kumpeleka Kituo cha Polisi cha Mailimoja, Kibaha,” alisema.
“Akiwa msituni alijisikia kupata fahamu, ambapo alianza kutambaa kuelekea barabarani ambako msamaria mwema mmoja alimuona na kisha kumpeleka Kituo cha Polisi cha Mailimoja, Kibaha,” alisema.
Alisema Polisi wa Kibaha ndio
waliochukua jukumu la kumpeleka katika Hospitali ya Tumbi saa nne usiku,
kabla ya kufanya uamuzi mwingine wa kuwasiliana na ndugu pamoja na
jamaa zake.
Kwa mujibu wa Bakari, polisi hao baada ya kufanya mazungumzo na ndugu wa Mgoba kwa minajili ya kumhamisha hospitali ili apatiwe matibabu zaidi, badala yake walimpeleka katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Bakari, polisi hao baada ya kufanya mazungumzo na ndugu wa Mgoba kwa minajili ya kumhamisha hospitali ili apatiwe matibabu zaidi, badala yake walimpeleka katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kilichopo jijini Dar es Salaam.
“Cha kushangaza huko Central walimuweka rumande na baadaye walimtaka atoe maelezo pasipo kujali hali aliyokuwa nayo,” alisema.
Alisema baadaye polisi huo walimruhusu Mgoba kuondoka na kumpatia Sh 2,000, ingawa wakati huo alikuwa akijisikia vibaya.
Inaelezwa kuwa baada ya kuruhusiwa
hakufika mbali, alidondoka na alizinduka akiwa amelazwa katika Hospitali
ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia
magari ya polisi (defender) matatu na basi moja la Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) yakiwa yameegeshwa katika viunga vya hospitali hiyo.
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani, Ulrich Matei, kuzungumzia tukio hilo, alikiri askari wake
kumpokea Mgoba na kisha kumpeleka katika Hospitali ya Tumbi baada ya
kumuona kuwa yupo katika hali mbaya.
Kamanda Matei alisema alipofikishwa katika hospitali ya Tumbi madaktari walithibitisha kuwa hana matatizo yoyote, na hivyo kuruhusiwa.
Kamanda Matei alisema alipofikishwa katika hospitali ya Tumbi madaktari walithibitisha kuwa hana matatizo yoyote, na hivyo kuruhusiwa.
“Polisi wangu walimsaidia kutafuta ndugu
zake na miongoni mwa waliofika ni mmoja aliyejitambulisha kama askari
polisi na mwingine Usalama wa Taifa, aliyejitambulisha polisi alidai
kuwa ni shemeji wa Mgoba, lakini yule aliyedai usalama wa Taifa alisema
ni ndugu yake kwa hiyo sisi tuliishia hapo, hayo mengine siyafahamu,
waulizwe polisi wa Dar es Salaam,” alisema Kamanda Matei.
Kamada wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Suleiman Kova, alisema ofisi yake ipo katika hatua za awali
za upelelezi na taarifa itatolewa leo ingawa kuna taarifa za kukanganya
kuhusu kijana huyo.
Daktari mmoja wa hospitali ya Amana
aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina alisema
mgonjwa huyo anaweza kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa kuwa
hospitali hiyo haina baadhi ya vipimo ambavyo vinaweza kubaini kitu
kilichotokea kwenye damu yake baada ya kulalamika maumivu sehemu za siri
na kudaiwa kuchomwa sindano.
RAIA TANZANIA
Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Rajab Mbarouk Mohamed amesema pamoja na mambo mengine, mbio za Urais ndani ya Chama cha CCM zimeifilisi nchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Rajab Mbarouk Mohamed amesema pamoja na mambo mengine, mbio za Urais ndani ya Chama cha CCM zimeifilisi nchi.
“Chanzo cha tatizo hili ni Serikali
kuingia kwenye miradi mikubwa inayohitaji fedha nyngi kwa wakati mmoja..
Kikubwa zaidi ni Uchaguzi Mkuu na dili za Urais ndani ya CCM. Hawa
jamaa wanakomba fedha nyingi kwa wakati mmoja..”– Mbarouk.
Mbarouk alitaja miradi iliyokwama kuwa
ni Bunge Maalum la Katiba, uandikishwaji wa daftari la Wapigakura, Kura
za Maoni uuandikishwaji wa Vitambulisho vya Taifa NIDA na Uchaguzi Mkuu
unaosimamiwa na NEC akisema hata huko fedha hazijaenda za uhakika.
Uchunguzi wa gazeti la RAIA TANZANIA
umebaini kuwa hali ya kifedha ndani ya Halmashauri ni mbaya na nyingine
zikitamani kufungwa, lakini alipotafutwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya
Salum alisema kucheleweshwa kwa fedha kunatokana na kitendo cha baadhi
ya Halmashauri kutorejesha maelezo ya matumizi ya fedha kutoka
Halmashauri husika.
NIPASHE
Hali ya afya za Watazania zipo hatarini kutokana na kasi ya kuingizwa dawa zisizofaa kwa tiba asilia kutoka nchi kadhaa za Asia hasa Korea Kaskazini.
Hali ya afya za Watazania zipo hatarini kutokana na kasi ya kuingizwa dawa zisizofaa kwa tiba asilia kutoka nchi kadhaa za Asia hasa Korea Kaskazini.
Uchunguzi wa Gazeti la NIPASHE umeonesha
dawa hizo zinaingizwa na kuuzwa nchini bila kuwa na maelezo yoyote ya
uthibitisho wa usalama wa dawa hizo pamoja na kuwa na ujazo wa madini
yanayozidi kiwango kinachotambullika kwa afya za watu.
Chanzo kimojawapo cha gazeti la NIPASHE
kilibaini kuwa dawa hizo zinauzwa na waganga wa jadi kutoka Korea
Kaskazini zilipaswa kuwa na viambata vya maelezo vilivyomo kwenye dawa
lakini hali haipo hivyo na wala hazina majina.
“Mimi ninasafirisha dawa zangu nje ya
nchi na huko lazima dawa iwe na jina, aina ya mti na uthibitisho kwamba
hazina sumu”– Maneno Tamba.
Akizungumza kwa niaba ya mtaalamu wa
masuala hayo Mwamaja amesema dawa zote zinaangaliwa na TFDA na sio
rahisi zikasajiliwa pasipo kukubalika na Mamlaka hiyo.
JAMBO LEO
Wanafunzi zaidi ya 503 wameshindwa
kuhudhuria masomo katika Shule ya Msingi Lengatei kutokana na mgogoro wa
mpaka uliopo kati ya Kijiji cha Lengatei na Zambia ambapo wazazi wa
wanafunzi hao waliwazuia watoto wao wasiende shule.
Ofisa ya Mtendaji wa Kijiji hicho Ezekiel Pingwa
amesema baadhi ya wazazi walivamia shuleni hapo na kuwacharaza viboko
na makofi wanafunzi akiwadia amri yao ya kutokuhudhuria shule.
Mtendaji huyo amesema sakata hilo la
mpaka linazidi kuchukua sura mpya baada ya Tume Maalum kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu kuweka mpaka katikati ya Shule hiyo jambo ambalo limepingwa
na wananchi hao.
MWANANCHI
Rais Kikwete amekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akichukua jukumu hilo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta aliyemaliza muda wake ambapo makabidhiano hayo yalifanyika jana katika mkutano wa 16 wa wakuu hao wa nchi hizo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Jomo Kenyatta.
Rais Kikwete amekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akichukua jukumu hilo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta aliyemaliza muda wake ambapo makabidhiano hayo yalifanyika jana katika mkutano wa 16 wa wakuu hao wa nchi hizo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Jomo Kenyatta.
Nchi hizo zilizindua mfumo wa
mawasiliano ya pamoja ambapo Rais Kikwete aliwasiliana na Balozi Sefue
na kuzungumza naye, kwa mfumo huo utaziwezesha nchi wanachama kupunguza
gharama za uendeshaji wa mikutano baina ya wajumbe ambapo awali wajumbe
walilazimika kusafiri na kukutana sehemu moja.
“Mfumo huu (video conferencing) utaondoa
haja ya wajumbe kukutana. Marais, mawaziri, makatibu wakuu pamoja na
wafanyakazi wa Serikali wataendesha mikutano yao bila ya kukutana. Hii
itapunguza matumizi ya fedha kwa ajili ya kujikimu na bajeti nyingine za
mikutano,”– Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Jamii Wizara ya
Ushirikiano Afrika Mashariki, Eliabi Chodota
Kuhusiana na katazo ambalo limetangazwa
na Kenya kwa gari za kitalii kuingia baadhi ya maeneo nchini humo,
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema hafahamu sababu ya
Kenya kuzuia magari hayo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment