HADITHI
YALIYONIKUTA TANGA (21)
IIPOISHIA TOEO IIOPITA
“Sawa. Leo kamilisha
taratibu za kuanza likizo, kesho utaondoka” afande wangu aliniambia.
“Nashukuru afande”
Nikamuaga na kutoka.
Siku ya pili yake
nikaanza likizo yangu. Na siku ya tatu nikaondoka kwenda Dar nikiwa
nimekichukua kile kisanduku cha dhahabu. Nilikitia kwenye begi langu.
Nilipofika Dar siku
iliyofuata nikatafuta usafiri wa kuelekea Kagera. Mpaka ninafika kijijini kwetu
ilinichukua siku mbili. Japo nilikuwa nimekutwa na madhila huko Tanga, nilipata
furaha kukutana tena na wazazi wangu pamoja na ndugu zangu ambao tuliachana kwa
karibu miaka mitatu iliyopita.
Iliuwa ni siku
iliyofuata nilipowakusanya ndugu zangu wawili ambao walikuwa wakubwa zangu
pamoja na wazazi wangu na kuwaeleza mkasa uliokuwa umenitokea huko Tanga.
Niliwaeleza wazi makosa
ambayo tuliyafanya mimi na Sajenti Erick ya kumbambikia kesi mwanamke ambaye
alikuwa ni jini baada ya kukataa kutupa rushwa. Lakini nilijitetea kuwa aliyepanga
mpango huo alikuwa mkuu wangu wa kazi ambaye alichinjwa kama kuku.
Pia nilificha kuwaeleza
habari ya kile kisanduku cha dhahabu ambacho nilikuwa nimekiiba nyumbani kwa
yule mwanamke na ambacho nilikwenda nacho Kagera.
Baada ya kuwaeleza mkasa
huo ambao uliwashangaza na kuwatia hofu, wazazi wangu waliniambia ni lazima
tutafute mganga tumueleze suala hilo halafu tumsikilize atatuambia nini.
SASA ENDELEA
Baada ya mazungumzo yetu
mama alinichukua tukaenda kwa mganga. Mganga mwenyewe alikuwa kijiji cha pili
na tulikwenda kwa miguu.
Wakati tunatembea pole
pole, mama aliniambia nilifanya vyema kuwahi kurudi kijijini hapo na kuwaeleza
mkasa huo kwani kama ningechelewa majini hao wangenichinja kama aivyochinjwa
Sajenti Erick.
“Tangu zamani tulikuwa
tunasikia sifa za mji wa Tanga, ni mji wenye majini wa hatari. Kumbe wengine
wanaishi na binaadamu na wanafanya biashara za dhahabu!” Mama aliniambia.
“IIitokea bahati kwamba
likizo yangu ilikuwa ipo tayari, nilicheleweshwa na hayo matatizo tu”
“Bahati yako mwanangu”
Tulipofika kwa mganga
nilishangaa kukuta mganga mwenyewe niiyesifiwa kuwa hodari kwa matatizo ya
majini alikuwa mwanamke tena akiwa bado msichana.
Hatukukuta watu,
tulikuwa ni sisi tu. Baada ya kusalimiana naye alitukaribisha ndani kwani
tulimkuta nje ya nyumba yake.
“Tumekuja tuna shida”
Mama alianza kumwambia mganga huyo mara tu tulipoingia kweye chumba chake cha
uganga kilichokuwa uani mwa nyumba yake.
“Shida gani?” mwanamke
huyo akatuuliza.
“Wewe ndiye mtaalamu,
tunataka utuambie shida yetu” Mama akamwambia.
“Mimi si mtaalamu, mimi
ni mtumishi tu wa wenyewe. Ngojeni niwaite mzungumze nao”
Mwanamke huyo baada ya
kutuambia hivyo alichukua upande wa kaniki akajifunika kisha akanusa ugoro. Baada
ya kuunusa mara tatu alipiga chafya kisha akatikisa kichwa chake kwa mfululizo.
Wakati anatikisa kichwa
alitupa mkono na kutusalimia kwa lugha ya kikwetu ambayo ndiyo iliyokuwa
ikitumika zaidi pale kijijini. Lakini wakati ule sauti yake ilikuwa imebadilika
na kuwa ya kiume.
Akatuambia kwamba
yeye ndiye mganga mwenyewe na amekuja kusikiliza shida yetu.
“Mimi ni jini wa kiti,
mwenye uganga huu. Nataka kusikiliza shida zenu” akatuambia.
“Tunataka ramli” mama
akamwambia.
“Oh mnataka
ramli…mtapata” akatuambia na kutazama juu ya dari ya miti ya chumba
tulichokuwemo.
Aliangalia boriti za ile
dari kwa sekunde kadhaa kama aliyekuwa akiangalia kitu kisha akakishusha kichwa
chake na kututazama.
“Ramli inakwenda kwa
kijana” akatuambia.
“Taire” Mama alitumia
neno la kinyumbani lenye maana ya neno hilo taire.
Mwanamke huyo aliinua
tena kichwa chake, safari hii hakuchelewa sana akakishusha taratibu.
“Nimeona” akatuambia na
kuongeza.
“Nimeona matatizo
makubwa sana, yametokea mbali na amekuja nayo hapa”
Mimi na mama
tukatazamana.
“Matatizo gani?” Mama
akauliza haraka.
Mganga akatazama tena
juu.
“Wewe na mwenzako
mlifanya makosa, naona damu nyingi…” akatuambia baada ya kukishusha kichwa
chake kisha akatazama tena juu.
Iikuwa kama vile pale
juu ndipo alipokuwa anasoma habari zetu.
“Mtu mmoja ameuliwa na
mmoja amechukua mali, ile mali ni ya majini” mwanamke huyo aliendelea
kutuambia.
Tukanyamaza kimya huku
tukiendeea kumsikiliza. Niishayatafsiri maneno yake kwamba mtu aliyeuliwa ni
Sajenti Erick na aliyechukua mali ni mimi. Mali ilikuwa ile dhahabu iliyokuwemo
kwenye kisanduku.
Mwanamke huyo baada ya
kutazama juu alishusha kichwa chake na kunitazama mimi.
“Hebu nieleze, nini
kimetokea” akaniambia.
Kwa vie aishaigusia
habari yenyewe nikaona nimueleze. Nikamueleza.
Mwanamke huyo akapiga
mluzi wa mshituko.
“Hatari!” akasema na
kuongeza.
“Wewe pia ungekufa. Umri
wako bado mrefu”
Akaendelea kutuambia.
“IIe nyumba inakaa
majini. Mwenyewe amekwishakufa. Majini wa pwani wanafanya biashara. Wewe
unapenda sana kutongoza wasichana. Sasa umetongoza jini. Alikuwa anakutafuta
akukomeshe”
Nilimuelewa
alichomaanisha. Alikuwa na maana kwamba mimi napenda kutongoza kwa sababu
nilimtongoza yule msichana wa kijini kwenye simu, kumbe msichana mwenyewe naye
alikuwa ananitafuta baada ya kumkamata mama yake na kumbambikia kesi ya uongo.
“Sasa nifanye nini ili
niweze kusalimika” nikamuuiza mwanamke huyo.
Niipomuuliza hivyo
alitazama juu. Baadaye aliurudisha chini uso wake akatuambia.
“Wenyewe wanataka
dhahabu yao”
“Hakuna namna ya kufanya
nikabaki nayo mimi?” nikamuuliza.
“Mimi utanipa nini?”
“Nitakupa pesa
utakayoitaka”
“Sawa. Kesho lete kile kisanduku,
nitakufanyia uganga wake. Hao majini hawatakufuata tena na wewe utabaki na
dhahabu yako”
“Hivyo ndivyo
ninavyotaka. Basi tutakuja kesho. Nitakileta na kile kisanduku” nikamwambia.
Yule jini alipoondoka,
yule mwanamke alituuliza tulichozungumza, tukamueleza.
“Sasa kesho mtakuja?”
akatuuliza.
“Tutakuja kesho asubuhi”
nikamjibu.
“Ngoja nikupe dawa
yangu” akatuambia na kuinuka.
Aikwenda pembeni mwa
chumba hicho. Alikuwa ameweka makorokoro yake ya kiganga. Akachukua pembe moja
ya mnyama aliyokuwa ameifunga kitambaa cheusi. Ule upande uliokuwa na shina la
ile pembe aliukung’uta kwenye kiganja chake, ukatoka unga mweusi.
Alinifungia unga huo
kwenye kikaratasi.
“Usiku utatia dawa hii
kwenye maji yako ya kuoga halafu utaoga” akaniambia.
Nikakichuku kile
kikaratasi na kukitia mfukoni.
“Niitie yote au
niibakishe?” nikamuuliza.
“Tia yote”
“Sawa”
Je nini kitaendelea?
Usikose kuendelea na hadithi hii katika toleo lijalo.
Niko tayari kukutumia habari inayonifia na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment