Pale ambapo mahubiri ya mama wa Mchungaji yanawakera wapita njia… Ishu mpaka Mahakamani
Mke huyo wa mchungaji ambaye amekutana
na mkasa huo Dakota, Marekani amepigwa faini hiyo baada ya kukutwa mara
kadhaa akihubiri barabarani jirani na makazi ya watu ambao nao waliwahi
kulalamika kwamba wanakerwa na kelele za mama huyo, mwisho wa siku
Polisi wa doria walimkuta na kumpeleka Mahakamani ambako alipigwa faini
ya dola 150 ambazo ni zaidi ya 270,000/- Tshs.
Mchungaji Juwle Nagbe
Mume wa mwanamke huyo Mchungaji Juwle Nagbe amesema mke wake amesikitishwa sana na maamuzi ya Mahakama hiyo.
Kanisa la Methodist lililopo Lisbon, Dakota Kaskazini, Marekani ambalo mume wa Martha ni Mchungaji wa kanisa hilo
Mbali na kupigwa faini hiyo Martha
amesema hatoacha kusali kwa sababu ana imani na MUNGU na pia anaamini
yuko huru kuendelea kufanya mahubiri kwa njia yoyote ambayo ataona iko
sawa na imani yake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment