Wanafunzi wamejikuta kwenye milango ya Gereza, kisa ni igizo lililoikwaza Serikali ya Thailand…
Wanafunzi
wawili Thailand wamejikuta wakiingia kwenye mikono ya Sheria kutokana
tu na igizo ambalo walitunga kwa ajili ya maazimisho ya miaka 40 ya
wanafunzi wa chuo hicho kupigwa na wanajeshi wa Thailand mwaka 1973
walipoandamana kudai demokrasia.
Maazimisho yao hayakuwa na heri kwa wanafunzi wawili Patiwat Saraiyaem na Porntip Mankong ambao waliandaa igizo hilo la jukwaani.
Igizo lilionekaa kukejeli uongozi wa
Mfalme wa nchi hiyo, kesi ikaenda Mahakamani wakahukumiwa kwenda
gerezani kwa miaka miwili na nusu kila mmoja, mchezo huo wa ‘The Wolf Bridge’ ulichezwa katika jukwaa la chuo kikuu cha Thammasat, Bangkok.
Hukumu ya wanafunzi hao ilikuwa kifungo
cha miaka mitano kila mmoja lakini walipunguziwa hukumu hadi miaka
miwili na nusu baada ya kukiri kosa.
“Mahakama
imejiridhisha kuwa ushiriki wao katika mchezo wa jukwaani
umeudhalilisha utawala wa kifalme, lakini baada ya kuirahisishia
mahakama kwa kukiri kosa tuliamua kuwapunguzia kifungo“; alisema Jaji wa Mahakama.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment