Korea wameamua hivi kuhusu ishu ya ‘kuchepuka’ kwenye ndoa…
Wakati TZ tunaendesha kampeni ya “Baki njia kuu..michepuko sio dili…epuka UKIMWI”
ili kuhimiza watu wajiepushe na mazingira yatakayosababisha kupata
maradhi hayo, leo ndio nafahamu kwamba kumbe Korea Kusin walienda hatua
nyingine mbele zaidi ya hii, wao walikuwa na Sheria ambayo ilikuwa mtu
ukikamatwa yani kwa kesi ya kuchepuka ni kama kesi nyingine tu,
unapelekwa Mahakamani na wengi wameshahukumiwa vifungo kabisa.
Ripoti inaonesha toka mwaka 2008 watu
zaidi ya 5,500 wamehukumiwa kwa kesi za kuwa na uhusiano nje ya ndoa,
jana historia imegeuka kwao, limekaa jopo la Majaji tisa, saba kati yao
wamekubali kuwa Sheria hivyo iondolewe.
Jaji Park Han-Chul
alikuwa mmoja ya walioshiriki kwenye jopo hilo, amesema imefika wakati
wa kubadili Sheria za masuala ya uhusiano wa kimapenzi kwa watu wao; “Hata
kama ishu ya kutoka nje ya ndoa ni kinyume cha maadili ya kijamii,
Serikali haipaswi kuingilia masuala ya maisha binafsi ya watu“– Park Han-Chul.
Sheria hiyo ilipitishwa mwaka 1953
ambapo hukumu ilikuwa kama ukikutwa na hatia ya kumsaliti penzi wako
kifungo ilikuwa mpaka miaka miwili jela.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment