Ni utaratibu wa jamii hii kukata vidole wakati wakiwa wanaomboleza msiba…
Utamaduni
wa watu duniani unatofautiana, moja ya story ambazo sikuwahi kufahamu
ni juu ya huu utamaduni wa jamii ya watu wa Dani iliyoko Magharibi mwa
Papua, New Guinea ambapo utamaduni wao unahusisha inapotoke msiba wa
ndugu yoyote basi ndugu wa marehemu wanaomboleza kwa kujikata vidole.
Hii imeshtua wengi walioisikia, kwa wale
waliobahatika kuitembelea basi ni mashuhuda kwamba watu wengi wa kutoka
jamii hiyo wamekatwa vidole na ndugu yoyote wa marehemu anakatwa
vidole, umri sio kitu kinachoangaliwa sana hivyo hata watoto pia
wanaguswa na hii moja kwa moja.
Utaratibu
huo huwa unakuwa na ibada ya utangulizi ili kufukuza mapepo ya marehemu
halafu linafuatia zoezi la kukata vidole, kwa utamaduni huo maumivu ya
mwili huonyesha huzuni ya kufiwa pamoja na kuonyesha upendo kwa
marehemu.
Hapa vidole vinakatwa kwa shoka, vipande
vilivyokatwa vinachomwa moto halafu majivu yanahifadhiwa au kuzikwa
pamoja na mwili wa marehemu.
Jitihada zimeanza kufanywa ili kuzuia utamaduni huo ambao madhara yake yameanza kuonekana kwa sasaNi halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment