Tangakumekuchablog
Lushoto,WAKULIMA
wa nafaka na mbogamboga kata ya Maore na
Kidundai Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, wameitaka Serikali kuwaajibisha maofisa
kilimo baada ya kushindwa kutekeleza wajibu
wao na badala yake wamekuwa
waking’ang’ania kukaa mjini.
Wakizungumza
katika mkutano wa wananchi leo, wakulima hao walisema kuna baadhi ya maofisa
kilimo ambao hawatekelezi wajibu wao na badala yake wanajifungia maofisini huku
wakulima wakishindwa kupata huduma za kitaalamu.
Walisema
wakulima wengi wamekuwa wakiendesha kilimo chao kwa hasara baada ya mazao yao
kushindwa kupata rutba na kuharibiwa na wadudu aina ya kiduha na magugu.
“Jitihada
za Serikali kuwapeleka wataalamu wa kilimo kila tarafa limekuwa msaada sana kwa
wakulima----ila kuna jambo ambalo bado haijalijua ambalo ni kuwa hawafiki
mashambani na badala yake wamekuwa wakijifungia maofisni” alisema Sued Bushir
“Nadhani
ni wakati sasa wa Serikali kutambua kuwa Lushoto ni eneo la wakulima wakubwa na
wenye bidii ya maendeleo----kila utupapo macho ni aina ya kilimo na hakuna pori
kwani ardhi yote iko na rutba” alisema
Kwa upande
wake mkulima wa njegere na mabamia, Ashraf Sadik,
ameiomba Serikali kuwapatia
soko la uhakika la kuuzia mazao yao na kuepuka ulanguzi kwa matajiri wenye
pesa.
Alisema
vipindi vya mavuno wamekuwa wakishuhudia kumiminika matajiri wakiwa na lengo la
kuwalangua wakulima baada ya kutokuwa na soko la uhakika la kuuzia mazao yao kama ilivyo kwa baadhi ya
Wilaya na Mikoa.
“Lushoto
hakuna kiwanda cha kusindika matunda na mbogamboga bali wapo wanaozuka vipindi
vya mavuno na kuwalalalia wakulima hasa wale wachanga” alisema Sadik
Akitoa
ushauri kwa wakulima wenzake , Sadik
aliwataka kuacha tamaa ya kuuza mazao yao kwa bei ya chini na kuwataka
kuwa na misimamo jambo ambalo litasaidia katika kukuza kilimo na kuwa mkulima wa kisasa.
Alisema
wako wakulima kwa mtazamo wamekuwa wakiuza mazao yao kwa bei ya chini jambo
ambalo limekuwa likiwakandamiza wakulima wenzao kila siku na kusababisha kuwa kuwa wanaweza kupoteza nguvu zao bila tija.
No comments:
Post a Comment