Sunday, February 22, 2015

SIKILIZENI UMEME WA REA UNAKUJA JAMANI


Wakazi wa kijiji cha Mailikumi kata ya Kwamsisi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, wakisikiliza maelekezo kutoka kwa maofisa wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) juu ya ujio wa mradi wa usambazaji umeme vijijini juzi.

  Injinia wa Miradi Tanecso Tanga, Kassim Rajab, akiwahutubia wananchi kijiji cha Mailimoja kata ya Mkwamsisi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga juzi wakati wa uhamasishaji wananchi kuupokea mradi wa umeme vijijini (Rea)

 Mkazi wa kijiji cha Mailimoja kata ya Kwamsisi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, Ibrahimu Bakary, akitaka ufafanuzi wa namna ambavyo wanaweza kupata unafuu wa uvutaji wa umeme kwa watu ambao wanakaa umbali na nguzo za umeme juzi wakati wa wafanyakazi wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) walipokuwa wakihamasisha wananchi kuupokea mridi wa usambazaji umeme vijijini Rea.
  Afisa Uhusiano na huduma kwa mteja, Monica Mabada , akizungumza wananchi wa kata ya Kwamsisi kijiji cha Mailikumi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakati wa uhamasishaji wananchi kuupokea mradi wa umeme vijijini (Rea) na kuepuka utapeli wa mafundi vishoka juzi.

No comments:

Post a Comment