Umeisikia hii ya msichana kukosa usingizi kwa miezi 11 baada ya kujifungua?
Binti huyo amesema kuwa hakuwa na tatizo lolote na alikuwa akiishi
vizuri na kufanya shughuli zake kama kawaida, lakini baada ya kujifungua
amejikuta na tatizo la kukosa usingizi wakati wote na kumfanya ashindwe
kulala kwa miezi kumi na moja kwa sasa na mwili wake hausikii wala
kuhisi kitu chochote.
Kutokana na tatizo hilo aliamua kwenda
Hospitali na kuambiwa kuwa ana tatizo la kurukwa akili, akapatiwa dawa
alizotumia kwa muda mrefu lakini bado hapati usingizi, kutokana na
tatizo hilo lililomfanya aishi kwa tabu kuna wakati alijaribu kujiua
zaidi ya mara tatu lakini ndugu zake walimuokoa na kwa sasa anahudhuria
Kanisani kwa ajili ya kufanyiwa maombezi.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment