
Timu ya
Arsenal usiku wa kuamkia leo iliendeleza kibarua chake cha kusaka tiketi ya kutinga hatua ya fainali katika mashindano ya kombe la
FA baada ya kuvaana na mahasimu wao wa kihistoria,
Manchester United kwenye uwanja wa nyumbani wa wakali hao wa
Old Trafford.
Katika mchezo huo
Arsenal ilifanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe hilo baada ya kuilaza
Manchester United kwa ushindi wa magoli 2-1.

Mchezaji wa zamani wa
Man United, Danny Welbeck aliifungia
Arsenal bao la ushindi katika dakika ya 61.
Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 25 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao
Nacho Monreal na baadaye
Man U wakasawazisha dakika ya 29 kupitia kwa nahodha wao
Wayne Rooney kabla ya
Welbeck kuhitimisha ushindi.
Angel Di Maria alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 77 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kumsukuma
Michael Oliver.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment