Sunday, March 8, 2015

BODABODA TANGA WATAKIWA KUACHA VILEVI WAKATI WA KAZI

Tangakumekuchablog

Tanga, MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Tanga, Kassim Mbuguni, ameutaka Umoja wa Madereva wa Bajaj na Pikipiki (Moperoo) kuwasimamisha uanachama madereva wanaotumia vilevi wakati wakiwa katika kazi lengo likiwa ni kupunguza ajali za barabarani.

Akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Umoja wa Madereva wa Pikipiki na Bajaj leo, Mbuguni alisema kuna baadhi ya madereva ambao hawathamini kazi yao na badala yake wamekuwa wakitumia vilevi wakati wakiwa kazini.

Alisema tabia hiyo imekuwa ikijengeka kwa baadhi ya madereva ambao wameivamia kazi hiyo na kushindwa kuithamini na hivyo kuutaka umoja huo kufanya kampeni ya kila dereva katika maegesho ya pikipiki zao.

“Sekta ya usafirishaji abiria bodaboda imekuwa kwa kasi na vijana wengi wamekuwa kimbilio---ila kuna baadhi yake wameivamia na hawakupitia mafunzo ya udereva “alisema Mbuguni na kuongeza

“Bodaboda kwa sasa  ni kazi yenye heshima tofauti na zamani wengi walikuwa hawajui wajibu wao na kudhani kama ni nguvu kazi kama nyengine---sasa mtu anavaa suti yake safi au sare yake akiwa nadhifu” alisema

Aliwataka kudumisha umoja na mshikamano na matatizo madogo madogo yamelizwe kwa taratibu na kuwataka kuwa na mawasuiliano na viongozi wao pamoja na walezi wa taasisi na vyama nyengine.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Mwenyekiti wa Moperoo, Silas Stivin, alimelitaka jehi la polisi kuwapatia redio za upepo (Radio Coll) ili kuweza kuwasiliana na wenzao wakati wa kazini na hasa wanaokodishwa kutoka nje ya mji.

Alisema maderava wengi wamekuwa wakifanya kazi zao kwa hofu ya kutekwa na kuibiwa pikipiki  kutokana na kutokuwa na mawasiliano na wenzao katika vituo.

Alisema kuwepo kwa utaratibu huo utasaidia kwa kiwango kikubwa kutokomeza utekaji na wizi wa pikipiki jambo ambalo pia watakuwa wanafanya kazi kwa amani hata katika mazingira ya kuogopesha.

“Kutokana na sekta ya usafirishaji abiria  kukua tunaomba Serikali kupitia polisi kutupatia radio za upepo ili kuweza kuwasiliana kituo kimoja na chengine ikiwa na pamoja na  kufanya kazi kwa amani” alisema Stivin

Aliwataka madereva hao kuheshimu sheria za barabani pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa wateja wao jambo ambalo litaweza kuongeza  kipato na uaminifu na kuwa na uhakika wa kufanya kazi.

                                          Mwisho



  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga, Kassimu Mbuguni (kulia)akikata utepe kufungua ofisi ya Umoja wa Madereva wa Bajaj na Pikipiki Tanga(Moperoo) iliyoko kata ya Mtupie Tanga jana, kushoo ni kamanda wa polisi wa usalama barabarani Tanga, Abdi Issango



Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga, Kassim Mbuguni pamoja na Madiwani na wenyeviti wa Serikali za mitaa kata ya Mtupie halmashauri ya jiji la Tanga wakiangalia pikipiki 10 zilizonunuliwa na Umoja wa Madereva  Tanga (Mopetoo)  ikiwa ni sehemu ya umoja huo kukopeshana ili kujikwamua na maisha tukio lililofanyika leo.

No comments:

Post a Comment