Monday, March 16, 2015

BODI YA PAROLE YAZINDULIWA

MAHAKAMA TANGA YAZINDUA BODI YA PAROLE



 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Magalula Said Magalula amewataka wajumbe wa Bodi ya Paroli Mkoa  kutenda kazi kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa ili  haki itendeke na kuepuka ushawishi wa namna yeyote katika kupokea na kuomba rushwa.

Hayo yamesemwa  wakati wa uzindua rasmi Bodi ya Parole Mkoa tukio lililofanyika katika ofisi za Magereza Mkoani humo.

Alisema  Lengo la Bodi hiyo ni  kuwajadili  wafungwa wenye sifa  za kuweza kuachiliwa huru baada ya kutimiza vigezo ambavyo vimeainishwa kwenye  sheria namba 25  ya Paroli ya mwaka 1994 na kufanyiwa mabadiliko mwaka 2002.

Alisema sheria husika imeweza kuanisha ni aina gani ya makosa ambayo mfungwa anaweza kupata fursa ya kuingia kwenye mpango wa Paroli . Pamoja na makosa hayo mfungwa hawezi kuingizwa kwenye utaratibu wa Paroli endapo amepatikana na kosa la unyang'anyi wa silaha, madawa ya kulevya, kulawiti, kubaka na mauaji ya kukusudia.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa sheria ya parole tangu utekelezaji wake mwaka 2003, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishina Agustino Mboje amesema tayari wafungwa 331 wameshaachiliwa huru kwa utaratibu wa parole, wafungwa 305 wamemaliza vifungo vyao salama na wafungwa 26 bado wanaendelea na vifungo vyao kwa utaratibu huu.

Licha ya kuwepo na mpango huu wa kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani lakini bado wafungwa wengi wameshindwa kunufaika na utaratibu wa Paroli kutokana na kutotimiza masharti ya parole.


 Maafisa wa Magereza wakimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Magalula Said Magalula
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kam. Augostino Mboje akitoa taarifa ya utekelezaji wa sheria ya Parole katika Mkoa wa Tanga
Baadhi ya wajumbe na Maafisa wa magereza wakati wa uzinduzi

No comments:

Post a Comment