Tuesday, March 3, 2015

G NAKO ALALAMIKIWA KUWATOZA FEDHA WASANII

Maneno ya G Nako kuhusu kutoza fedha   pamoja na kuingia kwenye sanaa ya uigizaji

.
.
Rapper kutokea kundi la Weusi, G Nako amefunguka kuhusiana na kuendelea kuwatoza fedha wasanii wanaomshirikisha katika nyimbo zao pamoja na kuingia kwenye sanaa ya filamu.
Akizungumza janaUamuzi wa kuwatoza fedha wasanii katika nyimbo zao wanazonishirikisha bado unaendelea ,unajua muziki wetu unapanua na watu wengi wanaujua kwa hiyo lazima sasa hivi tuwe katika level za kimataifa,  japokuwa bado katika steji ya kuwaweka watu sawa wasiwe wageni sana na hiki kitu kwasababu unaweza ukatoka kama msanii kwenda nchini nyingine ukashangaa lakini sio kitu cha kushangaa ni kitu cha kawaida kabisa..’–alisema G Nako
Mbali na kutoza fedha wasanii katika nyimbo anazoshirikishwa akagusia pia kuhusiana na kuingia kwenye sanaa ya  uigizaji.
‘Unajua kwenye sanaa kuna mahusiana  kati ya vitu viwili ambazo ni muziki na filamu kwa hiyo mashabiki wasishangee kuniona kwenye TV kuna short clips nimeigiza kwenye hiyo series ila bado haijatoka tuko kwenye maandalizi ya kuelekea kumalizia’–alisema G Nako.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment