Ishu ya Mama Maria Nyerere, kuzushiwa kifo, Mbunge Zitto Kabwe, Meya na pikipiki zake 420,
Kwenye zilizopewa Headlines Magazetini leo MARCH 11 kuna hizi;
Jeshi la Polisi kufuatilia TCRA nani aliyezusha ujumbe wa kumzushia kifo Mama Maria Nyerere, CHADEMA kumsimamisha uanachama Zitto Kabwe,
EWURA wameshauriwa kuhakikisha bei ya mafuta inapungua kulingana na
soko la dunia, watu 15 kushikiliwa na Jeshi la Polisi Rukwa kwa kuhusika
kumkata kumkata mkono mtoto Baraka Cosmas ambaye ni mkono mlemavu wa
ngozi.
TANESCo imeshauriwa kuboresha huduma
zake kwa kuwafuata wateja wake walipo, baraza la maadili limeombwa
kupendekeza adhabu kali kwa Meya wa Tabora anayemiliki mali mbalimbali
ikiwemo pikipiki 420, watoto 18 waliokutwa kwenye nyumba moja huko Moshi
kwa lengo la kufundishwa masomo ya dini limeendelea kuzua maswali,
muimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mbasha amesema mahakamani mtoto mchanga aliyenae ni mtoto halali wa mume wake Emmanuel Mbasha.
Iko pia stori ya Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta kuzuia mabehewa 124 kuingia Tz hadi uchunguzi wa tuhuma za ufisadi utakapokamilika.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment