Wednesday, March 4, 2015

JAMAA AJICHIMBIA CHUMBA CHA RUBANI NA KUGOMA KUSHUKA NDANI YA NDEGE, MAREKANI

Pale ambapo jamaa anagoma kutoka ndani ya chumba cha Rubani kwenye ndege…

cockpit_cover
Kwenye story ambazo zinahusu matukio ya kushtua na kushangaza kwa upande mwingine ni hii ya jamaa ambaye aligoma kushuka kwenye ndege baada ya ndege hiyo kutua, story ikazidi ukubwa baada ya jamaa huyo kwenda kujificha katika chumba  ambacho wanakaa marubani.
Maofisa wa usalama wa Uwanja wa ndege New York walitumia nguvu kumtoa jamaa huyo ambaye anaishi New Jersey , muda wote aligoma kushuka kwenye ndege akidai kwamba kuna kundi la watu walikuwa wanataka kumdhuru.
.
Ndege ya Shirika la ndege la Jetblue Airways ambayo jamaa alikuwa amejificha ndani.
Baada ya kutolewa alipelekwa Hospitali ya Jamaica ili kumcheki kama ana tatizo lolote la akili huku wakimfungulia mashitaka kwa kufanya kosa hilo.
Ndege hiyo ilitua New York ikitokea Jamhuri ya Dominica.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment