Pale ambapo kiazi kinatumika kama njia ya kupanga uzazi wa mpango..
Msichana huyo alisema alishauriwa na
mama yake kuweka kiazi sehemu zake za siri kama njia ya uzazi wa mpango
kuzuia asipate ujauzito.
Binti huyo amesema mama yake ndiye
aliyemuonesha njia hiyo ya asili kwa maelezo kwamba kiazi kinapoingizwa
sehemu za siri ni njia nzuri ya uzazi wa mpango.
Baada ya kupita wiki mbili alianza
kulalamikia maumivu yasiyokuwa ya kawaida na kuamua kwenda clinic, baada
ya kufanyiwa uchunguzi aligundulika mizizi inayochipua ikichungulia
kutoka kwenye sehemu zake za siri, lakini kiazi hicho kiliondolewa bila
kupata athari zozote katika njia yake ya uzazi.
Njia zisizo sahihi na hatari za uzazi wa
mpango bado zinaendelea kutumika ulimwenguni kote hasa na mabinti
wadogo wanaojihusisha na uhusiano wa kimapenzi kabla ya wakati.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment