Wednesday, March 11, 2015

MWANASHERIA WA ZITTO KABWE NGANGARI

Info ya mwisho kusikika inahusu taarifa zilizochukua headline jana kwenye vyombo vya habari juu ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, baada ya kutolewa kwa hukumu ya kesi aliyokuwa ameifungua kupinga CHADEMA kujadili uwanachama wake, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lisu amesema, wamemshinda kesi aliyofungua na kutokana na katiba ya chama hicho Zitto sio mwanachama wa chama hicho tena.
E. Wakili Abert Msando.Wakili za Zitto, Alberto Msando amesema kilichotokea sio hukumu kwasababu kesi ya msingi bado haijasikilizwa, ila kulikuwa na mapingamizi ya awali kuhusu uhalali wa kesi ya msingi kuwepo mahakamani ndicho kitu Mahakama imetolea maamuzi kwamba, pingamizi la awali linamantiki kuwa kesi hiyo ilitakiwa ifunguliwe Mahakama ya chini na sio hukumu kama inavyosemekana kwa kuwa, kesi ya msingi bado haijasikilizwa na hawakuwa na taarifa za kesi hiyo kusomwa jana, kwa sasa wanaangalia nini cha kufanya ili waweze kujiridhisha, kuhusu kuvuliwa uwanachama wake amesema tamko hilo limewasikitisha na halijafata utaratibu lakini kunauwezo wa kupeleka swala hilo Mahakamani na kuomba zuio la muda hadi kesi itakaposikilizwa ili aendelee kuwa mwanachama.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment