Tuesday, March 10, 2015

RIHANA NA NA WASHABIKI WAKE KILA KONA

Shabiki wa Rihanna kaamua kujioneshea upendo wa nguvu kwa hizi tattoo..

riri23Mapenzi ya mashabiki kwa mastaa mbalimbali huwa yanaonekana kwa njia nyingi, wengine wanavaa kama mastaa hao, wengine wananyoa, au kusuka.. Yani shabibiki anafanya chochote ili kuonyesha jinsi ambavyo ana mapenzi na staa huyo.
saraaHuyu ni shabiki wa nguvu wa Rihanna, ameamua kujichora tattoo 14 mwilini mwake kutokana na mapenzi aliyonayo kwa mwanamuziki huyo.
riri24
Sara Ridge ni shabiki huyo raia wa Afrika Kusini, ana tattoo saba zenye sura ya Rihanna katika mwili wake na ametumia zaidi ya paundi 2,000 kama gharama ya kujichora, katumia saa zaidi ya 48 mpaka zoezi lote limekamilika.
Mbali na picha hizo sehemu nyingine amechora maandishi ya mashairi ya nyimbo za staa huyo.
rrrrMama yake Sarah alimkataza mwanae kuchora tattoo hizo akimsihi kwamba huenda siku moja akajutia kufanya hivyo.
ririi22
Marafiki zangu na ndugu zangu hawakukubaliana na maamuzi yangu lakini kwa kuwa mwenyewe nilitaka kufanya hivyo, sikupenda kusikiliza ushauri wa mtu yoyote… siwezi kuja kujutia“– Sara.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia  www.tangakumekucha.blobspot.com

No comments:

Post a Comment