Tangakumekuchablog
Tanga, JAMII imetakiwa kuwa na mshikamano
katika kujiletea maendeleo na kuacha
mifarakano isiyo na tija jambo ambalo linaweza kurejesha nyuma nguvu kazi
katika kujileta kipato.
Akizungumza
katika mkutano mkuu wa mwaka, Umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waishio Tanga jana, mgeni rasmi katika mkutano huo, Simba Msuya,
alisema vikundi vya umoja ni jambo muhimu na lenye kuleta maendeleo.
Alisema umoja
ndani ya taasisi na jamii za watu ziko na msaada mkubwa katika kuharakisha
maendeleo yakiwemo ya elimu na vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira
magumu.
“Fursa ya
kuwa mgeni rasmi katika mkutano huu wa mwaka wa umoja wa wanamwanga ni jambo la
kufurahisha na kuweza kutoa neno ambalo linaweza kuwa msaada kwa wengine”
alisema Msuya na kuongeza
“Mimi
niwaombeni katika umoja wenu huu pia iwe msaada kule mutokako kwa kusaidia
shughuli za maendeleo kama upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati” alisema
Alisema
imekuwa ada kwa baadhi ya watu wanaounda umoja kuacha kuchangia huduma za maendeleo katika
maeneo yao na hivyo kusema kuwa huko hakutoweza kuleta maana ya umoja wao.
Akizungumza
katika mkutano huo, Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo, Yahya Mruma, alisema
wanachama wake wamekuwa wakishiriki katika kazi za maendeleo zikiwemo za ujenzi
wa maabara.
Alisema
wamekuwa wakishiriki kikamilifu ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali na
nguvu za wananchi katika ujenzi wa taifa na kuhakikisha malengo ya Serikali
yanatimia.
“Mbali na
kazi za umoja wetu lakini pia tumekuwa tukishiriki katika kazi za maendeleo
kama ujenzi wa maabara kwa baadhi ya shule hapa Tanga na kule Mwanga” alisema
Mruma
Amevitaka
vikundi vyengine vinavyounda umoja kutumia fursa wanazozipata kusaidia jamii na
kushiriki katika kazi mbalimbali za maendeleo ili kurahisisha huduma maeneo
yao.
Mlezi wa Umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waishio Tanga, akizungumza katika mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika ukumbi wa Tanga hoteli jana.
Mwanachama wa umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waisho Tanga , Geofrey Msuya, akitoa ushauri wa jambo katika mkutano mkuu wa mwaka wa umoja huo uliofanyika jana Tanga.
No comments:
Post a Comment