Australia wanahalalisha matumizi ya Bangi? Hiki ndio kinachofatia kwa sasa..
Kuna idadi kubwa ya Majimbo Marekani wao
hawana tatizo kabisa na masuala ya Bangi… imehalalishwa na inapatikana
Madukani kama bidhaa nyingine za kawaida, sio nchi nyingi ambazo
zimekubaliana kuhalalisha Bangi, Tanzania nayo imo.
Australia walianzisha Kampeni mwaka 2013
kuishawishi serikali ibadilishe Sheria ili kuhalalisha matumizi ya
Bangi, majibu yaliyopatikana miaka miwili baadaye yani mwaka 2015 ni
kwamba zaidi ya watu 246,000 wanahitaji Sheria irekebishwe na Bangi
iruhusiwe kwa ajili ya kusaidia watu wenye matatizo na wanaohitaji Bangi
kama tiba !!
Serikali ya Australia imeamua
kulishughulikia hilo, kwa sasa wako kwenye mpango kuruhusu Bangi itumike
kwa matumizi ya Matibabu, Sheria iliyopo kwa sasa hairuhusiwi kulima,
kutumia au kukutwa na Bangi.. ukikamatwa ni kifungo au faini ambayo
inatofautiana kutokana na Kanuni za Jimbo husika.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment