Kilichonifikia kutoka Kenya kuhusu Helikopta waliyopata nayo ajali Marehemu Filikunjombe..
Bado Tanzania iko kwenye Majonzi siku moja baada ya Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Haule Filikunjombe, Rubani Captein William Silaa, na watu wengine wawili, Egid Nkwera pamoja na Cassablanca Haule.
Taarifa nyingine imeandikwa kuhusu
Helicopter ambayo Marehemu hao wanne wamepata nayo ajali katika Mbuga ya
Selous, kwenye Stori hiyo ametajwa Mwanasiasa mkubwa Kenya ambaye pia
ni mmoja ya Viongozi wa Muungano wa Vyama vya CORD, Kalonzo Musyoka kwamba ndiye mmiliki wa Helicopter hiyo ambaye aliikodisha TZ katika msimu huu wa Kampeni.
Helicopter hiyo aina ya Eurocopter AS 350B3 Écureuil ilinunuliwa
na Mwanasiasa huyo mwaka 2013 wakati wa shughuli za Uchaguzi Mkuu Kenya
na baada ya hapo alikuwa akiikodisha kwa watu mbalimbali mpaka October 15 2015 ambapo ilipata ajali na kuteketea kwa moto katika Mbuga ya Selous na kusababisha Vifo vya watu hao wanne.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment