Tangakumekuchablog
Mkinga, UCHAGUZI
Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, umekuwa wa kihistoria baada ya wananchi wengi
kujitokeza katika vituo vya kupigia kura na kusababisha baadhi ya huduma muhimu
ya usafiri wa magari yaendayo mjini na Wilayani pamoja na bodaboda kusitishwa.
Kabla ya kuanza kupiga kura mamia
katika vituo vilikuwa vimefurika watu wakiwa wamejipanga foleni kwa utulivu na mara maofisa wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kuanza uchaguzi huo ulienda vizuri.
Kituo cha mabasi yaendayo mjini na
vijijini vilikuwa vyeupe pamoja na maegesho ya pikipiki maarufu kama bodaboda
pamoja na wafanyabiashara wenye maduka kufunga maduka yao ili kutekeleza haki
yao ya kupiga kura.
Mkazi wa mtaa wa Mabatini Sokoni
Maramba B, Juma Khamis, alisema alipanga kwenda Tanga mjini ili aweze kurudi na
kuweza kupiga kura lakini alipofika kituo cha magari hakukuta gari hivyo
kuahirisha.
“Nilipanga niende mjini kumuona
ndugu yangu ambaye amelazwa hospitali ili
nirejee jioni kabla ya muda wa mwisho wa kupiga kura lakini sijakuta gari hata
moja” alisema Khamis na kuongeza
“La kushangaza ni kuona hata
bodaboda nao hawapo katika maegesho yao----inamaanisha nao wamenda kupiga kura
na kuonyesha uchaguzi huu ni wa aina yake” alisema
Katika kata ya Mwakijembe, watu
wengi walijitokeza kupiga kura na kuacha shughuli zao zote bila kujali jua kali
ambalo lilikuwa linapiga huku baadhi ya wanawake wakiwa na watoto mgongoni.
Wanawake wengi wamejitokeza kupiga
kura huku wakiwa na watoto wao migongoni na baadhi yao kupewa kipaumbele cha
kuingia chumba cha kupigia kura pamoja na wazee na wagonjwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment