Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI la
Polisi Mkoani Tanga limesema limejiandaa kukabiliana na makundi ambayo
yataonyesha kufanya fujo siku ya uchaguzi kesho na kuwataka wananchi kupiga
kura na kuendelea na majukumu yao ya kujiletea maendeleo.
Akizungumz ana waandishi wa habari (leo) , kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, aliwataka wananchi kupiga
kura na kurejea maeneo yao ya kazi na kudai kuwa yoyote ambaye atakiuka sheria
atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema polisi itakuwa makini na
kikundi au mtu yoyote ambaye atafanya fujo na hivyo kuwataka wananchi
kutekeleza haki zao za kisheria za kupiga kura na kuwataka kufuata sheria.
“Ndugu waandishi wa habari kupitia
kwenu naomba kuwaomba wanachi kutumia haki yao ya kuchagua kiongozi wanaemtaka
kwa amani na utulivu kama uliopo----yoyote ambaye atakiuka sheria tutamchukulia
sheria” alisema Mombeji na kuongeza
“Nendeni katika vituo vya kupigia
kura na kasha rejeeni katika majukumu yaenu ya kujiletea maendeleo----musiwe na
wasiwasi kama eti kutatokea fujo kwa kweli tumejipanga na kujidhatiti kwa
atakaeleta fujo” alisema
Kamanda Mombeji aliwataka wananchi
kuepuka mikusanyiko ya watu wengi kwani siku hiyo hawataruhusu mikusanyiko na
hivyo kutakuwa na doria kila pembe na mitaa.
Alisema mikusanyiko yoyote polisi
itaichukulia kama ni haramu hivyo ili kuweza kuepuka ni wajibu wa kila mmoja
kuhakikisha anapiga kura na kwenda katika sehemu yake ya kazi ama kurejea
majumbani.
Mwisho
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji akizungumz ana waandishi wa habari leo kuzungumzia juu ya usalama wananchi na mali zao ikiwa na pamoja na kusema kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kukabiliana na vurugu zozote ambazo zitatokea na hivyo kuwataka wananchi kupiga kura na kwenda katika shughuli zao za ujenzi wa Taifa
No comments:
Post a Comment