Tangakumekuchablog
Tanga, MGOMBEA
Ubunge jimbo la Tanga mjini kupitia ACT-Wazalendo, Ahmed Kidege, amevitaja
vipaumbele vyake vinne endapo atachaguliwa kuwa Mbunge kuwa ni Elimu, Ajira, Afya na Miundombinu na kuwataka
wananchi kumuamini.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara mtaa wa Madina kata ya Mikanjuni, Kidege alisema anatambua wananchi
shinda zao na hivyo vipaumbele hivyo ni ndio ufumbuzi wa maisha hivyo kuwataka kutofanya makosa.
Alisema vijana wengi hawana kazi na
wamekuwa wakizurura mitaani na baadhi
yao kujitumbukiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na kufanya vitendo vya
uporaji na wizi wa mifukoni.
“Ndugu zangu wamepita wagombea wengi
kuomba kura kwenu lakini hakuna hata mmoja mweye vipaumbele vitakavyomuondolea
umasikini mwananchi----nasema hivi kwa kuamini nina uwezo” alisema Kidege na
kuongeza
“Nichagueni mimi Kidege na acheni
ushabiki wa vyama ambavyo havina sera wala muelekeo---ushabiki wenu utakuja
kuwagharimu na kuja kunikumbuka ni mimi ni mimi Kidege jamani” alisema
Alisema atahakikisha hakuna mtoto
atakaeshindwa kwenda shule kwa sababu ya sare au vifaa vya shule hivyo mfuko wa
Mbunge utahudumia wanafunzi wa msingi na sekondari.
Alikitaja kipaumbele chengine kuwa
ni ajira ambapo atahakikisha hakuna kijana anaezurura mitaani kwa kukosa kazi
ya kufanya na hivyo atanzisha miradi ya ujasiriamali kwa kuanzisha vikundi vya
vijana.
Kipaumbele kingine alikitaja kuwa ni
afya ambapo atatenga vitengo maalumu kwa wanawake na wanaume pamoja na wazee
kwa kudai kuwa ni kuondosha kero ya misongomano wakati wa kuhitaji matibabu.
Alisema katika vituo vya afya na
zahanati amedai kuwa hakuna utaratibu wa kijana, mzee wala mtoto hivyo na
kusababisha kero na kutojulikana mgonjwa wala mzima.
Mgombea huyo wa Ubunge alikitaja
kipaumbele cha nne kuwa ni miundombinu na kusema kuwa atahakikisha barabara
zote za mjini zinakuwa katika kiwango cha lami na zile za nje ya jiji ataziweka
vifusi ziweze kupitika na kuwawezesha wakulima kupeleka mazao yao katika
masoko.
Aliwataka wananchi wa jimbo hilo
kumchagua kwa kura nyingi na kuacha ushabiki wa vyama kwa madai kuwa yuko na
uzoefu wa kuongona kiutawala hivyo Mbunge anaefaa ni yeye tu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment