Tangakumekuchablog
Tanga, MGOMBEA
Ubunge jimbo la Tanga mjini, Mussa Mbarouk (CUF) amewataka wananchi kumpa
ridhaa ya kuwa Mbunge wao na kusema kuwa ahadi zote alizozitoa atazitekeleza
kwani yuko na uwezo nao.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara wa kuomba kura leo barabara ya 13 Ngamiani kati, Mussa aliwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kumchagua kuwa Mbunge wao
ili kuufufua uchumi wa Tanga.
Alisema baada ya kufa kwa viwanda
uchumi wa Tanga umekufa na kusababisha wafanyabiashara na wawekezaji kuukimbia
mji huo na hivyo kuwataka wananchi kumchagua ili kuweza kuirejesha Tanga katika
ramani yake katika uchumi.
“Ndugu zangu wananchi wa Tanga
nawaombeni sasa sana musije fanya makosa kwa kumchagua mwengine asie kuwa
mimi---kila mtu ni shahidi seheme zote za viwanda sasa ni magofu na maficho ya
vibaka” alisema Mussa na kuongeza
“Ahadi zangu nilizozitoa mwanzo wa
kampeni zangu hadi hii leo ni za ukweli na niko na uwezo ndio
nikazitangaza----ili munipime na kunisuta jaribuni kunipa ubunge na kuona” alisema
Nae mgombea Udiwani kata ya Ngamiani
kati kupitia CUF, Habib Mpa, alisema safari hii CCM imekabwa pabaya na hivyo
haiwezi kufurukuta havyo wananchi kutegemea ushindi wa mwaka.
Alisema Chama hicho kimefikia kikomo
cha kuongoza hivyo kutakiwa kuwekwa kwanzo na kuweza kujipanga upya na kusubiri
mwaka 2020 endapo kitakuwepo na kuingia ulingoni.
“Wananchi wenzangu tuwe na
utulivu mara baada ya kupiga ili CCM
wasije kusema sisi tumefanya fujo kwani wameshajitambua kuwa hapa hawana chao”
alisema Mpa
Alisema CUF iko na uhakika wa
kulinyakua jimbo hilo hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kila
mmoja aliejiandikisha kuhakikisha atapiga kura na kumchagua Lowassa, Mussa na
Habib Mpa ili kuweza kutengeneza timu ya maendeleo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment