Papa Francis kuweka historia leo
Historia ya kanisa katoliki inatarajiwa kuandikishwa upya leo na Papa Francis huko Vatican.
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis anatarajiwa kuwatawaza mume na mke kuwa watakatifu.
Louis na Zelie Martin walikuwa wapenzi waloishi katika karne 19.
Watano waliojaliwa kuishi hadi kuwa watu wazima waliishia kuwa watawa wote.
Mdogo zaidi kati yao ndiye aliyepata umaarufu zaidi na alifahamika kwa jina la Theresa kutoka Lisie
Shughuli hii ya leo itafanyika katika ukumbi wa kanisa hilo huko Vatican ambapo mkutano wa viongozi wa kidini au makadinali unaendelea.
CHANZO BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment