Tangakumekuchablog
Bumbuli, MGOMBEA
Udiwani kata ya Vuga jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Dhahabu
Jumaa kupitia CCM, amesema endapo atachaguliwa kuwa Diwani atahakikisha kero ya
maji inapatiwa ufumbuzi sambamba na kiwanda cha kusindika matunda..
Akizungumza katika mkutano wa kuomba
kura leo kijiji cha Vuga juu, Dhahabu, alisema anatambua kero za wananchi wa
kata hiyo hivyo kuwaomba kumchagua kwa kura nyingi ili kuwatatulia na kudai
kuwa muarobaini wa kero hizo yuko nazo.
Alisema hakuna sababu ya wakulima
kuwa masikini na kuwa mitaji kwa matajiri na badala yake atawashirikisha
wafadhili na wawekezaji wa ndani na nje
kujenga kiwanda cha kusindika matunda ndani ya kata hiyo inayongoza kwa
kilimo cha mbogamboga na matunda .
‘Ndugu zangu mimi ni kijana wenu
mdogo mtiifu nisie na makuu si kwa kijana wala mzee----kwa maana hiyo nawaomba
munichague kwa kura nyingi kuwa diwani wenu” alisema Dhahabu na kuongeza
“Muarobaini wa soko la kuuzia mazao
yenu pamoja na kiwanda cha kusindika matunda ni mimi Dhahabu----si munaliona
jina langu liko juu zaidi ya lulu na almasi” alisema
Alisema kwa kutumia uzoefu wake na
mahusiano mazuri na viongozi na wafadhili wan je atahakikisha kiwanda cha
kusindika matunda kinajengwa ndani ya kata hiyo ambayo amedai kuwa ndio
inayongoza kwa kilimo cha mbogamboga.
Akizungumzia kuhusu barabara ,
mgombea huyo alisema atatengeneza miundombinu ya kuwawezesha wakulima
mashambani wanayafikia masoko kwa urahisi hata nyakati za mvua.
Alisema kwa sasa njia nyingi
zimekuwa kero kutoa mazao mashambani kutokana na mvua zinazonyesha na njia
kusababisha matope na magari kukwama na
hivyo kusema kuwa atazichonga ili ziweze kupitia nyakati zote za mvua na jua.
“Mukinichagua kuwa diwani wenu kero
ya wakulima kutoa mazao yao mashambani nyakati za mvua zitaisha----nitazichonga
ili kupitika nyakati zote iwe mvua au jua” alisema Dhahabu
Aliwataka wananchi wa kata hiyo
kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura na kumchagua kwa kura nyingi ili kuwa Diwani wao na kuweza kuwaletea maendeleo na kudai kuwa
ofisi yake muda wote itakuwa wazi kupokea kero za wananchi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment