Tangakumekuchablog
Tanga, KAMISHNA
wa Tumeya Taifa ya Uchaguzi, Mjaka Mchanga, amesikitishwa na mwenendo wa
kampeni za uchaguzi majukwaani na kuwaomba wagombea kuacha kutoa maneno makali
na badala yake kutangaza sera za vyama vyao.
Akizungumza katika kongamano leo na
viongozi wa vyama vya siasa ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa, Mchanga,
alisema Tume inasikitishwa kuona baadhi ya vyama kutumia majukwaa vibaya.
Alisema kipindi kilichobaki kuelekea
uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani ni fursa ya kipekee kwa wagombea
kujinadi kwa sera nzuri ambazo zitawavutia wananchi.
“Ni fursa ya kipekee kwa viongozi wa
siasa hapa Tanga kukutana hapa na kujadili mambo ya msingi kuelekea
uchaguzi----natambua wengi wenu hapa ni
wagombea au wakikilishi wa wawagombea” alisema Mchanga na kuongeza
“Tume inasikitishwa na mwenendo wa
kampeni majukwaani ----baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa maneno yasiyo mazuri
kwa washindani----hebu zitumieni siku hizi chache zilizobaki kutoa sera
zitakazowavutia wapiga kura” alisema
Mchanga amewataka wagombea pamoja na
wanasiasa kuyatumia majukwaa yao kuzungumzia suala zima la amani pamoja na
kunadi sera zao kwa wananchi ili kuweza kuwavutia na kuvuna wapiga kura.
Kwa upande wake Mgombea Udiwani kata
ya Mwanzange, Rashid Jumbe wa Chama Cha Wananchi (CUF) ameitaka tume hiyo
kusimamia uchaguzi kwa haki na amani bila ushabiki wa chama chochote.
Alisema vipindi vya uchaguzi Tume ya Uchaguzi imekuwa ikilalamikiwa katika
mchakato mzima wa uchaguzi na hivyo kuitaka tuhuma hizo kuzifuta na badala yake
kusimamia kwa haki .
“Mheshimiwa kamishna wa tume ya
uchaguzi taifa kwa heshima na taadhima naiomba tume yako kusimamia kwa haki
uchaguzi huu kwani tumezoea kuona uvurugwaji kuanzia upigaji kura hadi
uhesabuji na utangazaji” alisema Rashid na kuongeza
“Hapa kwetu hakuna dalili za
viashiria vya fujo wala zogo----ila natoa angalizo simamieni uchaguzi ili uwe
huru na haki kwa kila chama kinachoshiriki uchaguzi kiridhike” alisema
Alisema uchaguzi wa mwaka huu ni wa
ushindani mkubwa kuliko chaguzi zote zilizopita hivyo kuitaka tume hiyo
kusimamia kwa haki bila upendeleo wa
chama kimoja .
Mwisho
Kamishna wa Chama Cha NCCR Mageuzi Mkoa wa Tanga, Ramadhani Manyeko, akichangia wakati wa mdahalo wa viongozi wa vyama vya siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi uliofanyika leo ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
Mgombea Udiwani kata ya Mwanzange kupitia CUF, Rashid Jumbe, akichangia wakati wa kongamano la viongozi wa vyama vya siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi lililofanyika leo ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mjaka Mchanga akifungua kongamano la viongozi wa vyma vya siasa leo ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu
No comments:
Post a Comment