Mtoto aliyekamatwa na saa wakidhani ni bomu amekaribishwa Ikulu ya Obama.. Mipango ya shule?
Unamkumbuka Ahmed Mohamed mtoto kutoka Dallas, Texas Marekani aliyekamatwa na polisi baada ya kupeleka shule saa iliyodhaniwa kuwa ni bomu? Yes, Ahmed aliweka headlines nyingi sana Marekani na
saa yake ambayo baadaye ilikuja kuonekana kuwa saa ile ilikuwa haina
madhara yoyote kitendo ambacho pia kilisababisha mshituko mkubwa sana
kwa mtoto huyo.
Headlines za Ahmed leo zipo tofauti sana, siku ya jumanne October 20 familia ya Ahmed ilitangaza maamuzi yao ya kuhamia Doha, Qatar baada ya taasisi inayoitwa ‘Qatar Foundation’ kutoa ofa ya kumlipia mtoto huyo malipo yote ya elimu yake ya sekondari mpaka degree yake ya kwanza!
Kwenye mazungumzo na waandishi wa habari nchini Marekani, familia ya Ahmed ilisema kwamba walipokea ofa nyingi sana za msaada baada ya stori ya Ahmed kuwafikia watu wa sehemu mbalimbali duniani na waliongeza kwa kusema kuwa wameamua kuchagua kwenda Doha, Qatar kwasababu wamefanya utafiti wao kama familia na wamegundua kuwa taasisi ya ‘Qatar Foundation’ ina histori nzuri ya kuwajenga vijana wadogo kwa kukuza utamaduni wa uvumbuzi na ubunifu.
>>> ”
Tunakamilisha mpango wa kuhamia Doha, Qatar ndani ya siku chache
zijazo, tumepokea ofa nyingi juu ya Ahmed baada ya watu wengi kuguswa na
stori yake lakini kama familia tumeona Ahmed atakuwa na fursa nzuri
zaidi akiwa Qatar kwani Qatar Foundation inatoa mchango mkubwa kwenye
kukuza utamaduni wa ubunifu na uvumbuzi kwa vijana wadogo kama Ahmed…” <<< maneno ya wazazi wake Ahmed kwenye The Dallas Morning News.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment