Tangakumekuchablog
Tanga,MGOMBEA
Udiwani kata ya Majengo Tanga mjini, Nassir Makata (CCM), amesema endapo atachaguliwa
atahakikisha barabara zote za vumbi ndani ya kata hiyo zinajengwa kwa kiwango
cha lami.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara wa kuomba kura Leo uliofanyika barabara ya 15, Makata alisema
maendeleo hayawezi kuwafikia wananchi
bila kuwa na barabara nzuri.
Alisema barabara zote ambazo ni za
vumbi na mashimo atahakikisha zinatengezewa kwa kiwango cha lami na hivyo
kuwataka wananchi kumchagua kwa kura nyingi ili aweze kuingia katika baraza la
madiwani na kuitekeleza ahadi yake hiyo.
“Ndugu zangu wananchi mimi ni kijana
wenu mtiifu na hakuna hata mmoja ambaye hanijui mei---nimekulia hapa hapa
nimesoma hapaha hata watoto mitaani wananijua” alisema Makata na kuongeza
“Nichagueni mimi niwatengenezee
barabara kwa kushirikiana na madiwani wenzangu na Serikali kwani bila nyinyi
sitoweza kufanikisha adhma yangu” alisema
Akizungumzia ajira kwa vijana,
mgombea huyo alisema ataunda vikundi vya ujasiriamali kwa na kuwapatia mikopo
ikiwa na pamoja na masoko ambayo watakuwa na uhakika wa kuuza bidhaa zao.
Alisema vijana wengi wamekuwa hawana
shughuli za kufanya wakati kazi ziko nyingi ila nyenzo wanashindwa kupata hivyo
kuwaahidi kumchagua na kumaliza kero yao.
“Vijana wenzangu natambua kuwa kero
yenu kubwa ni ajira ambayo kwa kipindi kirefu ndio kilio chenu----muarobaini
wenu ni mimi kwa kunichagua kwa kura nyingi kuwa mwakilishi wenu” alisema
Makata
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa
wingi siku ya kupiga kura wake kw waume walemavu na wazee ili kumchagua na
kuweza kuwa mwakilishi wao ndani ya kata na kutoa ahadi kuwa kero zao
atazishughulikia .
Mwisho
No comments:
Post a Comment