Thursday, October 22, 2015

WAANDISHI WA TANGA WAPEWA SOMO


Tangakumekuchablog
Korogwe, WAANDISHI wa habari wa Mkoani Tanga wametakiwa kuandika fursa za uwekezaji zilizoko Mkoani humo zikiwemo bandari na vivutio vya kitalii ili kuweza kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika kongamano la wadau wa habari na waandishi wa habari wa Mkoani Tanga jana Wilayani hapa, Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari Tanga, Moni Msemo, aliwataka waandishi hao kuitumia kalamu ya kwa maendeleo ya Tanga.
Alisema Tanga iko na fursa nyingi za kimaendeleo ikiwemo bandari na vivutio  vya kitalii lakini havitangazwi hivyo kuwa sababu ya maendeleo Mkoani humo kudidimia na kuwataka waandishi haoi kuitumia vyema kalamu zao kwa kuitangaza Tanga
“Leo ni bahari kukutana nanyi tena kwa asilimia tisini na tano mupo hapa----tumejaliwa kuwa na bandari na vivutio vya kitalii munajua kuwa nje ya mkoa wetu hakuna anaejua” alisema Msemo na kuongeza
“Hebu jamani zitumieni kalamu zenu kuitangaza bandari ili hata wafanyabiashara wan je waje kushusha shehena zao kwetu tutambue kuwa uchumu wetu utakuwa na ajira kuongezeka” alisema
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji (Tanga Uwassa), Dora Killo, aliwataka waandishi wa habari kutobweteka na viwango vya elimu walivyofikia na badala yake wasome ili wawe waandishi mahiri wenye kufuata weledi wa upashaji habari.
Alisema kuna baadhi ya waandishi  wamekuwa wakiandika habari zisizofuata maadili ya habari na hivyo kuingia katika matatizo na wadau wa habari pamoja na wamilikiki wa vyombo hivyo.
Alisema ili kumfanya mawandishi kuwa mahuiri ni vyema kutobweteka na mafanikio yaliyofikiwa na badala yake wasome ili kuweza kuyafikia malengo katika tasnia hiyo.
“Ndugu zangu waandishi wa habari ninyi ni watu muhimu katika suala zima la kuelimisha jamii----mimi kama mwakilishi wa mamlaka ya maji bila nyinyi hatuwezi kufika kama tulipofikia” alisema Killo
Alisema mamlaka ya maji Tanga Uwassa, imekuwa ikiwashirikisha mara kwa mara katika shughuli zake na kila palipo na malalamiko hushirikisha waandishi ikiwa lengo ni kuweka mahusiano mema kwa mamlaka na wateja wao.
                                                   Mwisho

  Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Wilaya ya Tanga, Hamis Ngoda, akichangia mada wakati wa kongamano la wadau wa habari na waandishi wa habari wa Mkoani Tanga (TPC) lilifanyika jana mji mdogo wa Hale Wilayani Korogwe.



Mwandishi wa habari wa Gazeti la Daily News, Nestory Ngwega, akichangia mada wakati wa kongamano la waandishi wa habari wa klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga (TPC)  na wadau wa habari lililofanyika jana mji mdogo wa Hale Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment