Tangakumekuchablog
Tanga,MGOMBEA
Udiwani kata ya Mikanjuni halmashauri ya jiji la Tanga , Mwinyi Kamari ( CCM), amesema endapo akichaguliwa
kuwa Diwani ataondosha michango isiyo ya
lazima shule za msingi na sekondari.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara jana mtaa wa Madina, Kamari alisema kipindi chake cha Udiwani
hatokubali kuona mwanafunzi amerejeshwa nyumbani kutokana na kushindwa kutoa
michango.
Alisema watoto wote watasoma kama
wengine na atanzisha mradi maalumu kwa wanafunzi wenye wazazi wenye kipato cha
chini ili kuwawezesha kusoma hadi masomo ya juu.
“Ndugu zangu wananchi mtaa huu wa
madina ambao mimi najiona kama niko nyumbani kwetu----nikiangalia nawaona
wajomba mashangazi na wazee wangu ambao najua wote watanipa kura zao” alisema
na kuongeza
“Sina shaka mwaka huu udiwani ni wa
kamari ambaye ndie mwenye haiba na mvuto kwa wananchi kwa kunichagua kwa kura
nyingi----nionavyo wala sina haja ya kupiga debe ila ni kupiga brashi “ alisema
Akizungumzia mazingira , Kamari
alisema atachimba mifereji ya kupitisha maji katika mitaa ambayo nyakati za
mvua inasababisha mafuriko kwa kuichimba na kuwa ya kudumu.
Alisema kuna baadhi ya maeneo ambayo
nyakati za mvua hutuwama na hivyo kuwataka wananchi kuungana kwa pamoja ili
kuweza kulimaliza tatizo hilo ambalo limekuwa likiwapa wakati mgumu wakati wa
mvua za masika na za mwaka.
Alisema mifereji mingi imeziba
kutokana na kutofanyiwa usafi hivyo akiwa Diwani atatoa ajira kwa watu ambao
wataweza kuhudumia mifereji na kuweza kujipatia vipato vyao kupitia mifereji
hiyo.
“Hakuana sababu ya vijana kwa wazee
kukaa bila kazi -----ziko kazi nyingi na mimi nikiwa diwani nitanzisha miradi
mbalimbali ikiwemo ya usafishaji mifereji” alisema Kamari
Aliwataka wananchi kumchagua ili
kuwa Diwani wao ili kuweza kuibadili kata hiyo ambayo iko nyuma kimaendeleo
ilhali iko na vyanzo vingi vya mapato na vijana kuweza kujiajiri.
Mwisho
No comments:
Post a Comment