Mgombea Urais kupitia CHAUMMA kayazungumza kuhusu kuanzishwa kwa chama chake pamoja idadi ya wabunge, madiwani…
Tukiwa bado kwenye headlines za Uchaguzi
2015 nakusogezea hii stori kutoka kwa mgombea Urais kupitia chama cha
Ukombozi wa Umma, Hasheem Rungwe.
‘Chama cha
Ukombozi wa Umma kilianzishwa mwaka 2012 lakini kilipata usajili 2013
mpaka leo hii kina uongozi wa kudumu na bahati nzuri mimi walinichagua
kuwa mwenyekiti wa chama, malengo ya chama chetu ni kuwakomboa
watanzania katika hali zao duni’- Hasheem Rungwe
‘Katika
msafara wangu wa kampeni zangu nilikuwa na magari mawili katika mikoa
mbalimbali na katika kampeni zangu nilikuwa napata watu walikuwa
wanakuja na wananisikiliza mimi mgombea wa Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma’- Hasheem Rungwe
‘Idadi ya
wadiwani na wabunge katika chama chetu kwanza sisi tumesimamisha wabunge
katika mikoa isiyozidi 18 na katika mikoa hiyo yote tuna wabunge na
tunao madiwani siwezi kukumbuka idadi yao lakini tunao madiwani Dar es
Salaam tuna madiwani Temeke, tuna madiwani Kinondoni’ – Hasheem Rungwe
‘Cha
mwisho ambacho ningependa kukisema ni kwamba wale wote waliopitishwa
kugombea Urais wanye kwenye mdahalo wazungumzie na asije mtu kumsemea
Fulani tunataka wagombea Urais tukutakane kwenye mdahalo ili wananchi
wafahamu nini watakachoamua tarehe 25 Octoba, maana nimesikia kuna
baadhi ya wagombea wanakwepa mdahalo, kwa hiyo mimi nataka mdahalo hata
sasa hivi’- Hasheem Rungwe
No comments:
Post a Comment