Tangakumekuchablog
Tanga,MGOMBEA
Ubunge jimbo la Tanga mjini, Mussa Mbarouk (CUF) amesema endapo atachaguliwa
kuwa Mbunge atahakikisha taa za
barabarani zinawaka usiku ili kuwawezesha
wafanyabiashara shughuli zao hadi usiku
na kuongeza kipato chao.
Akizungumza katika mkutano wa
kampeni jan barabara ya 15 kata ya Majengo, Mussa alisema jiji la Tanga
limepoteza hadhi yake kutokana na kutokuwa na taa za barabarani na kusababisha
giza nyakati za usiku.
Alisema awali jiji hilo lilikuwa
likipendezeshwa na taa za barabarani nyakati za usiku jambo ambalo lilikuwa
likiwawezesha wajasiriamali wanawake na wanaume kufanya biashara zao za kuuza
samaki na maandazi na kupunguza umasikini majumbani.
“Ndugu zangu wananchi wa jimbo la
Tanga nawaomba musifanye mchezo katika kuchagua viongozi ambao watawatatulia
kero zenu zaidi ya viongozi wa ukawa----nichagueni mimi kwani uwezo wa kuongoza
niko nao” alisema na kuongeza
“Mukinichagua nitalirejesha jiji
letu katika muonekano kama wa zamani mataa yote barabarani yatawaka na kuwa
kama majiji mengine nyakati za usiku-----taa zipo sijui kwa nini
haziwashwi---nasema mimi nitaziwasha” alisema Mussa
Kwa upande wake mgombea Udiwani kata ya Majengo, Suleiman Idd, alisema endapo
atachaguliwa kuwa Diwani, atahakikisha kodi ya usafi wa mazingira unaondoshwa
pamoja na kodi za leseni za biashara ndogondogo ikiwemo uuzaji wa kahawa na
biashara za mikononi.
Alisema kodi hizo zimekuwa kero kwa
wafanyabiashara wadogowandogo wa kuuza kahawa barabarani pamoja na karanga hivyo kuwataka wananchi kumchagua kwa kura
nyingi.
“Ndugu zangu mimi ni kijana wenu
mtiifu na kila mmoja hapa ananitambua utendaji wangu ----- sina shaka
mutanichagua kwa kura nyingi na nitawalipa fadhila kwa kuwaondolea kodi za
kupandikiza” alisema Idd
Alisema atasimamia maendeleo ya kata
yake kwa kuhakikisha usafi wa mazingira na wafanyabiashara hawasumbuliwi na
askari mgambo katika kazi zao za kujipatia kipato.
Mwisho
No comments:
Post a Comment