HALI YA UNYONYESHAJI WATOTO NCHINI SIO NZURI
Mwakilisha
wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Maniza
Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili
kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama
kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto
nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog)
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline
Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF akielezea hali ya
unyonyeshaji kwa watoto ilivyo nchini.
Imeelezwa
kuwa wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita
nchini sio mzuri na hivyo kuwa na uwezekano wa watoto kudhoofika kwa
kukosa maziwa ya mama ambayo yanakuwa na virutibisho muhimu kwa ukuaji
ya mtoto.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe,
Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili
kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama
kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
Dkt.
Kaganda amesema wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi
sita ni asilimia 42 na wastani huo ni mdogo hivyo kuashiria kuwa hali
sio njema kwa watoto ambao hawapati maziwa ya mama.
Amesema
kiafya inatakiwa mtoto aanze kunyonya nusu saa baada ya kuzaliwa na
mtoto anyonye maziwa ya mama yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita
na baada ya hapo anaweza kuanza kuwa anachanganya na vyakula vingine
kama uji na maji.
“Hali
sio nzuri ukiangalia wastani wa wamama ambao wanawapa watoto wao maziwa
ya kunyonya ni wachache na labda inawezekana wengi wakawa hawatambui
matatizo yanayoweza kutokea kama hawatawanyonyesha watoto wao,” amesema
Dkt. Kaganda.
Aidha
Dkt. Kaganda amesema kazi zinachangia kina mama wengi kushindwa
kuwanyonyesha watoto wao lakini wanaweza kuweka utaratibu wa kuwa
wanakamua maziwa yao na kuyahifadhi sehemu nzuri ili hata kama
wanapokuwa mbali na watoto wao, msimamizi anayemuangalia mtoto aweze
kumpa mtoto ili kumfanya apate virutubisho muhimu kutoka kwenye maziwa
ya mama yake.
Nae
Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,
Bi. Maniza Zaman amesema katika kusaidia Tanzania kuongeza wastani wa
watoto ambao wananyonya wamekuwa wakitoa elimu kwa kina mama
wanaonyonyesha pamoja na familia zao ili wajue umuhimu wa mtoto kunyonya
maziwa ya mama.
Alisema
watoto wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa matatizo ambayo yanatokana
na kukosa maziwa ya mama zao na hivyo ili kuzidi kushughulikia tatizo
hilo wanataraji kuanza kutoa elimu kwa watumishi wa afya katika mikoa ya
Mbeya, Iringa na Njombe na wanataraji kutembelea zaidi maeneo ya
vijijini kutokana maeneo hayo kuonekana kutokuwa na elimu hiyo zaidi.
“Watoto
wamekuwa wakipata matatizo na kupoteza maisha na hiyo inachangiwa na
kutokunyonya kwa mama … tumeshirikiana na serikali tunataraji kutoa
elimu katika vijiji zaidi ya 15,000 kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na
Mbeya na tutafundisha pia mama na familia umuhimu wa mtoto kunyonya,”
alisema Bi. Zaman.
Alisema
baada ya kumalizika kwa mikoa hiyo wataendeleza utoaji wa elimu nchi
nzima ili jamii ya Tanzania itambue umuhimu wa watoto kunyonya maziwa ya
mama na pia kuwaomba waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika
jamii ili kuwaelimisha watanzania kuhusu tatizo hilo.
Katika
makala zilizoandikwa katika jarida la habari za afya la The Lancet
linaonyesha kuwa uboreshaji wa kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza
kuokoa maisha zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za
Kimarekani Bilioni 302 kila mwaka.
Imendaliwa na Rabi Hume wa Modewjiblog
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa.
Mshauri
Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao
Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akielezea kuhusu makala za
The Lancet juu ya uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya
mama jinsi kunavyoweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha
ya watoto nchini.
Mshauri
Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao
Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa
warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet
linalohusika na kuandika habari za afya.
Viongozi
wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakifatilia ripoti
ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet. Wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya
Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline
Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto
(UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
Mkurugenzi
Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza
idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto.
Viongozi
wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakisikiliza maswali
yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wa sekta ya afya na waandishi wa habari.
Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na
unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin,
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya
Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline
Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto
(UNICEF) nchini, Maniza Zaman.
Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo.
Mwakilisha
wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Maniza
Zaman akitoa neno la shukrani kuashiria kumalizika kwa warsha