Tangakumekuchablog
Korogwe, MBUNGE wa
jimbo la Korogwe Vijijini, Stivin Ngonyani, maarufu kama Profesa Majimarefu,
ametoa jezi seti tano, mipira mitatu vyenye thamani zaidi ya shilingi laki 5
kwa timu ya mpira ya vijana wa Makuyuni Wilayani Korogwe lengo likiwa ni kukuza
vipaji.
Vifaa hivyo kwa mujibu wa Mbunge
huyo vimekuja kufuatia maombi ya vijana wa Makuyuni kumtaka kusaidia ili kuweza
kuimarisha timu yao na kuingia ligi ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.
Alisema msaada huo hautoishia hapo
lakini atapenda kuona timu hiyo inafanya vizuri ligi ngazi ya Tarafa na kuahidi
kuisaidia kwa hali na mali hivyo kuwataka kuonyesha moyo na mapenzi na timu.
“Leo nawapeni jezi na mipira
kumaliza kilio chenu kwani nakumbuka barua yenu muloniandikia nikiwa bungeni na
mukaiacha kwa katibu wangu pale ofisini, niwaahidi kuwa mimi kama mbunge wenu
nitakuwa nanyi bega kwa bega” alisema Majimarefu na kuongeza
“Nitahakikisha timu yenu inaingia
mashindano ya Wilaya hadi mkoa na mimi kuwa mlezi wenu na musisite kunieleza
kwa lolote” alisema
Kwa upande wake Kocha wa timu hiyo,
Mbaraka Kiondo, alimshukuru mbunge huyo na kusema kuwa msaada wake huo aloutoa
utatumika kama ilivyo na kumuahidi kuwa hawatamuangusha katika mashindano ya
ligi.
Alisema awali walikuwa wanatumia
mipra mmoja huku wakiwa hawana jezi na badala yake kila mchezaji alikuwa
anatumia fulana yake jambo ambalo lilikuwa kero wakati wa uchezaji na
kutoelewana.
“Mheshimiwa Mbunge hatuna la
kukulipa na hatuna la kusema kwani hatujui tuanze wapi ila nimalize kwa kusema
asante sana na Mungu ndie atakakulipa na kukubariki” alisema Kiondo
Aliwataka wachezaji wake kuzingatia
muda wa kufanya mazoezi baada ya kupata vifaa hivyo na kuwataka kupiga kambi
ili kushikilia usukani wa ligi hiyo ngazi ya Tarafa na msimu wa ligi kuingia
ngazi ya Wilaya.
Mwisho
No comments:
Post a Comment