Tangakumekuchablog
Tanga, MAMLAKA
ya Chakula na Dawa Tanga imeteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani zaidi ya
shilingi milioni 14 zilizopitwa na
wakati katika ukaguzi mpaka wa Horohoro na Kenya pamoja na madukani.
Akizungumza mara baada ya kufanyika
zoezi la uteketezaji, Meneja kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Chakula na dawa
(TFDA), Dammas Matiko, alisema miongoni mwa vyakula na bidhaa hizo ni nyama za mbuzi na ng’ombe, vipodozi pamoja na vinywaji vikali zikiwemo bia.
Alisema ukaguzi huo ulikuwa na
changamoto nyingi zikiwemo wafanyabiashara kukataa kukaguliwa na bidhaa zao
kuzificha maeneo ambayo ni vigumu kuonekana kwa urahisi.
“Kwa juma zima tumekuwa tukifanya
ukaguzi wa kushtukiza katika maduka
hoteli na machinjio, tumefanikiwa kugundua machinjio ya kienyeji mitaani
ambayo hayakubaliki ksheria” alisema Matiko na kuongeza
“Ukaguzi huu wa kushtukiza utakuwa
endelevu hadi pale tutakapojiridhisha hakuna bidhaa zilizopitwa na wakati na
vyama ambazo hazijathibitishwa” alisema
Matiko amewaonya wafanyabiashara
kuacha kuagizia bidhaa ambazo zimepitwa na wakati na kusema kuwa sheria
haitomvumilia mtu yoyote na badala yake
itawatetea walaji ambao ndio wahanga.
Kwa upande wake Afisa kitengo cha
Usalama wa Chakula, dawa na vipodozi halmashauri ya jiji la Tanga, Alice
Maungu, amewataka wananchi kuwa na kawaida ya kusoma tarehe za kutengezwa na
kuisha muda wa bidhaa anayonunua.
Alisema Watanzania wengi hawana ada
ya kujua bidhaa siku iliyotengezezwa jambo ambalo limekuwa likiwaathiri ngozi
zao au kuugua magonjwa ambayo chanzo chake ni matumizi ya bidhaa zilizoisha
muda wa matumizi.
“Watu wengi hawana kawaida ya kujua
bidhaa anayoinunua iko hai au imekufa, hili ni tatizo na ndio maana tunawapa
kiburi wafanyabiashara kuagizia bidhaa zilizopitwa na wakati” alisema Maungu
Alisema ni wajibu wa kila mteja
anapoenda kununua bidhaa dukani kuangalia tarehe siku iliyotengenezwa na mwisho
wa matumizi ikiwa ni kukaribisha matatizo wakati wa matumizi.
Mwisho
Watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga, wakikusanya mapande ya nyama ya ng’ombe na mbuzi zilizokamatwa sokoni na kuzichoma moto jana dampo la Mwang’ombe baada ya kubainika nyama hizo ziko na magonjwa katika zoezi lilifanywa kwa siku tatu mfululizo kwa usimamizi wa Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Kaskazini, Dammas Matiko .
Meneja kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dammas Matiko, akimwaga bia zilizokamatwa katika baa mbalimbali Tanga ambazo zimeisha muda wake wa matumizi zoezi lililofanyika kwa siku tatu mfululizo na kuzitekelezwa dampo la Mwang’ombe jana
Meneja kanda ya
Kaskazini Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dammas Matiko (kushoto) na Afisa
Afya kitengo cha usalama wa chakula na dawa halmashauri ya jiji la Tanga, Alice
Maungu (kulia) kwa pamoja wakiteketeza makopo ya rangi zilizoisha muda wake wa
matumizi dampo la Mwang’ombe Tanga jana
No comments:
Post a Comment