CONFIRMED: Pep Guardiola kathibitishwa kujiunga na Man City
Kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania Pep Guardiola ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani, February 1 ameingia kwenye headlines baada ya muda mrefu kuthibitisha kuwa ataondoka FC Bayern Munich lakini hakuwa ameweka wazi klabu gani atanenda kujiunga nayo.
Manuel Pellegrini
February 1 ikiwa zimesalia saa kadhaa kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa, klabu ya Man City imetoa statement rasmi kuwa Pep Guardiola atajiunga na klabu yao na tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia klabu hiyo.
Statement ya Man City iliyotolewa kuthibitisha Pep Guardio;a kujiunga na Man City mwisho wa msimu.
Hivyo Pep Guardiola atarithi mikoba ya kocha wa sasa wa Man City Manuel Pellegrini mwishoni mwa msimu huu. Sehemu ya Statement iliyotolewa na klabu hiyo inaeleza kuwa Man City imefikia makubaliano na Pep Guardiola ya kujiunga na kuifundisha Man City msimu wa 2016/2017.
Takwimu za Pellegrini akiwa na Man City
Rekodi ya ukocha wa Pep Guardiola akiwa katika vilabu vya FC Bayern Munich na FC Barcelona
No comments:
Post a Comment