Tangakumekuchablog
Mlalo, MBUNGE
wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi,(CCM) amewataka wakulima wa mbogamboga na
matunda Wilayani Lushoto kulichangamkia soko la pamoja la Afrika Mashariki na
kuacha kusubiri walanguzi wa mazao yao mashambani.
Akizungumza na wakulima wa Mlalo, Bumbuli na Lushoto jana wakati wa kikao cha wadau wa
kilimo cha mbogamboga na matunda, Shangazi alisema wakulima wengi hawana
taarifa la soko la pamoja hivyo kutakiwa kuelimishwa.
Alisema ni wakulima wachache ambao wako
na uelewa wa soko hilona wengi wao wakiwa hawana uelewa ambalo kwa miaka mingi
wamekuwa mtaji wa matajiri na kurudisha nyuma sekta ya kilimo cha mbogamboga na
matunda Wilayani humo.
“Kuna soko la pamoja ambalo
limefunguliwa zamani tu, nashangaa sioni mkulima hata mmoja hapa anaepeleka
mazao yake moja katika soko linalounda umoja huo zaidi ya wenzetu tu” alisema
Shangazi na kuongeza
“Nchi zetu moja ya malengo yake ni
hizi za kuwasaidia wakulima na wajasiriamali kutangaza kazi zao na kuuza katika
masoko na kuweza kuongeza kipato cha kazi zao pamoja na kujifunza” alisema
Shangazi alisema ofisi yake ya Ubunge imejipanga kuhakikisha mkulima wa mboga
mboga na matunda anayafikia masoko ili kuweza kujinasua na ukiritimba wa
kulanguliwa bei na wafanyabiashara wenye pesa.
Kwa upande wake mkulima wa nyanya na
maboga, Shembilu Saleh, alisema wakulima wengi wanakabiliwa na changamoto ya
kuweza kuwakabili wadudu waharibifu wa
mazao baada ya gharama za madawa kuwa bei ya juu.
Alisema ni vyema Serikali kupunguza
gharama za uagiziaji wa madawa ya wadudu wa mbogamboga na matunda kwani wengi
wao wamekuwa wakishindwa kumudu na badala yake hulima kilimo cha kubahatisha.
Alisema wakulima wengi ni wakulima
wa kipato cha chini ambao hulima kwa jembe la mkono hivyo kushindwa kumudu gharama za kununua madawa na
mbolea ya mimea yao.
“Sisi wakulima wadogo wa jembe la
mkono hatuna mabadiliko kila misimu ya mavuno, kwanza tuko na changamoto za
madawa ya wadudu kwani gharama ziko juu” alisema Saleh
Ameiomba Serikali kuwaokoa wakulima
wadogowadogo kwa kuwawezesha kupata dawa za wadudu kwa gharama nafuu ili kuweza
kufikia malengo yao na kuwa wakulima wa kisasa na kuachana na kilimo cha jembe.
Mwisho
No comments:
Post a Comment