Lionel Messi kaifunga Arsenal Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuvunja rekodi yake hii kwa Cech
Usiku wa February 23 klabu ya FC Barcelona ya Hispania ilikuwa imesafiri kutoka Hispania hadi London Uingereza kukutana na Arsenal katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya klabu Bingwa barani Afrika, mchezo ambao ulikuwa wa hatua ya 16 bora, hivyo kila timu ilikuwa inahitaji ushindi.
Mchezo ulimalizika kwa Lionel Messi kuipatia FC Barcelona ushindi wa goli 2-0, magoli ya Lionel Messi yaliofungwa dakika ya 71 na 83, yalifanya mitaa mbalimbali ya London Uingereza kupooza, kwani ndio makazi ya mashabiki wengi wa Arsenal.
Kwa matokeo hayo Arsenal italazimika kwenda Nou Camp kusaka ushindi wa zaidi ya goli mbili ili iweze kuiondoa FC Barcelona na wao watinge robo fainali. Hata hivyo ushindi wa goli mbili kwa Lionel Messi dhidi ya kipa wa Arsenal Petr Cech, unavunja mwiko wa Messi kutowahi kumfunga Petr Cech kwa jumla ya muda wa masaa 10 na dakika 11.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment