Mvuto wa ramani za viwanja 12 vitakavyotumika Kombe la Dunia 2022 Qatar
Kwa kawaida maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia
hufanyika miaka zaidi ya minne kabla ya nchi husika kuanza kupokea timu
katika miji yao. Imekuwa kawaida kwa kila nchi inayotarajia kuwa
mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia kutengeneza viwanja vipya na
vyenye hadhi kwa ajili ya michuano hiyo.
Nchi ya Qatar ambayo ndio mwenyeji wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022 mtandao wa sokka.com
umetoa list pichaz 12 za viwanja vinavyotajwa kuwa vitatumika katika
mihuano hiyo 2022. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee pichaz 12 za
muonekano wa viwanja 12 vilivyotajwa na sokka.com kuwa vitatumika 2022.
1- Lusail Iconic Stadium
Huu
upo mji wa Al-Daayen na unamilikiwa na kamati ya Olympic ya Qatar na
una uwezo wa kuchukuwa mashabiki 86,250, utattumika katika mechi za
makundi ya michuano hiyo, 16 bora, robo fainali, nusu fainali na
fainali.
2- Khalifa International stadium
Upo
mji wa Al-Rayyan na unamilikiwa na serikali na kamati ya Olympic
unauwezo wa kuchukua mashabiki 50000. Utatumika katika mechi za makundi,
16 bora, robo fainali na nusu fainali.
3- Sports City stadium
Utachezewa mechi za makundi na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu upo mji wa Doha na unauwezo wa kuchukua mashabiki 47,560.
4-Al-Khor Stadium
Hiki
pia kinamilikiwa na serikali pamoja na Qatar Olympic Committee kipo mji
wa Al-Khor kitatumika kuchezea mechi za makundi na 16 bora pia kina
uwezo wa kubeba mashabiki 45,330.
5-Al-Shamal Stadium
Huu
utachezewa mechi za hatua ya makundi lakini unamilikiwa pia na Serikali
ya Qatar pamoja na Qatar Olympic Committee. Upo mji wa Al-Shamal
unauwezo wa kuchukua mashabiki 45,120.
6-Al-Wakrah Stadium
Mji
wa ambao Al-Wakrah upo uwanja huu utapata nafasi ya kuona mechi za
makundi na 16 ya michuano hiyo. Unamilikiwa na Serikali ya Qatar na
Qatar Olympic Committee ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 45,120.
7-Umm Slal Stadium
Mji
wa Umm Slal utapata nafasi ya kushuhudia mechi za makundi, 16 bora na
robo fainali zitakazochezwa katika uwanja huo. unamilikiwa na serikali
ya Qatar na unauwezo wa kuchukua mashabiki 45,120.
8-Doha Port Stadium
Mji
wa Doha ndio kipo kiwanja hiki kinachomilikiwa na Serikali ya Qatar
kitatumika katika mechi za makundi, 16 bora na mechi za robo fainali.
kinaripotiwa kuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 44,950.
9- Education city stadium
Hiki
ni kiwanja kingine kilichopo Al-Rayyan Qatar ambacho kitatumika katika
michuano hiyo. Uwezo wake wa kuchukua mashabiki ni 45,350.
10-Al-Gharafa Stadium
Kipo mji wa Al-Rayyan na kitatumika katika mechi za hatua ya makundi pekee. Uwezo wa kuchukua mashabiki ni 21,282.
11-Al-Rayyan Stadium
Hiki
ni kiwanja kingine kitakachotumika katika michuano hiyo kipo katika mji
wa Al-Rayyan, huu ni uwanka ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua
mashabiki 21,282.
12- Qatar University Stadium
Doha kutakuwa na uwanja mwingine utakaotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2022 ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 43,520.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa Tangakumechablog
We just wanted to say Property Hunter shifted this service to a level much higher than the broker concept.
ReplyDeleteyou can see more details like this article Properties For Sale in pearl Qatar