Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI la
Polisi Mkoani Tanga, limewakamata wahamiji haramu 13 wenye asili ya Ethopia
waliofichwa msitu wa Kirare kata ya
Pongwe Tanga huku afya zao zikiwa mbaya baada
ya kutembea siku 30 toka waianze safari nchini kwao Ethopia.
Wahamiaji hao ambao wote wamechoka
na baadhi yao kushindwa kutembea kutokana na kukaa na njaa na kudai kuwa
wamekuwa wakinywa maji ya mito huku madali wao wakiwashindisha na njaa.
Walisema kwa siku zote 30 toka
waianze safari wamekuwa wakipita pori kwa pori kuanzia nchini Ethopia , Mombasa
nchini Kenya na kuingia Tanzania na kufika mahala kujutia safari yao huku
kutojua pa kuanzia safari ya kurejea kwao.
Mmoja wa wahamiaji haramu hao ambaye
ndie pekee aliekuwa akizungumza kiarabu alisema wanashukuru askari wa Tanga kwa
kuwakamata kwani wameijutia safari yao ambayo jua mvua ni la kwao huku
wakishindwa kupata fursa ya kuoga, kupiga mswaki na kulala pahala salama.
Ameitaka Serikali kupitia ofisi ya
kamanda wa polisi Tanga kuwarejesha nyumbani kwao ili kuona na familia zao na
kujutia kwa madai kuwa hakujua kama safari hiyo itakuwa ya madhila.
Alisema kwa siku zote hizo wamekuwa
wakila mizizi na majani pamoja na matunda ya msituni ambayo hawayajui huku
madali wao wakiwafuata usiku kila siku wakiwa na maji tu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment