Tuesday, February 23, 2016

KINGI AJIPA MATUMAINI KIBAO



Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA Mkuu wa Muheza United, John Kingi, amesema kipigo walichokitoa kwa Small Prison ya Tanga ni salamu kwa wapinzani wao watakaokutana fainali na kutoa salamu kuwa  kombe la ligi ngazi ya Mkoa litaenda Muheza.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kipenga cha mwisho uwanja wa Mkwakwani juzi, Kingi aliwapongeza wachezaji wake na kuwataka kuongeza mazoezi bila kukosa i na morali wa ushindi siku ya fainali  Febr 28.
Alisema mchezo huo ulipoanza  alikuwa na hofu kutoka na wapinzani wao kutumia pasi ndefu  na mipira ya juu hivyo kuubadilisha kwa kutumia mfumo wa 3, 5 , 2 na kuwachanganya wachezaji wa Small Prison.
“Mpira ulipoanza tu nilingia hofu kwa mfumo wao wa kutumia pasi ndefu na pasi za juu, ndipo wachezaji wangu nikawapanga kwa mfumo mwengine na kupata mabao ya chap chap” alisema Kingi na kuongeza
“Sasa mawazo na akili yetu iko kwenye fainali ambayo tunakutana na majirani zetu wa Korogwe United, tunawajua kuwa ni wazuri sio wa kuwabeza ila niseme kuwa nasi tunajipanga” alisema
Alisema kwa sasa wataweka kambi (hakuitaja) kuhakikisha wachezaji wake wanafanya mazoezi mfululizo na kuwajenga kimwili na kimchezo hadi siku ya fainali na kombe hilo kwenda Muheza.
Kwa upande wake, kocha wa Small Prison ya Tanga, Msafiri Hassan, amemlaumu refarii na kusema aliwanyima nafasi za kufunga ila kwa sasa anajipanga msimu wa ligi kwa kufanya usajili wa nguvu.
Alisema mwamuzi aliwanyima nafasi za kuelekea kufunga mara tatu na kusema mazingira hayo yaliwanyong’onyeza wachezaji wake na kupoteza morali wa uchezaji uwanjani.
“Tuseme ligi imeisha licha kuwa tutacheza na Jeshi Worrias kusaka nafasi ya tatu, malengo yetu ilikuwa ni kuingia fainali na matokeo ndio kama haya yaliyotokea kwa kweli inauma sana” alisema Hassan
Alisema kipindi cha kuisha kwa ligi kazi ambayo ataifanya ni kutafuta wachezaji wenye kipaji ili kukisuka kikosi ambacho kitakuwa moto na kuhakikisha kombe hilo liwe la kwao.
Alisema usajili wake hautokuwa mkubwa kama watu wanavyofikiria bali kutakuwa na mabadiliko madogo sehemu ya beki, kiungo na ushambuliaji na kudai kuwa hatakurupuka kufanya usajili huo.
                                                       Mwisho

 Wachezaji wa Muheza United, wakijadiliana uwanjani wakati wa mchezo na Small Prison  ligi ngazi ya Mkoa uwanja wa Mkwakwani juzi na kufanikiwa kutinga fainali baada ya kuifunga mabao 2, 0.

 Wachezaji wa Small Prison wakigombea mpira na wachezaji wa Muheza United  ligi ngazi ya Mkoa juzi Uwanja wa Mkwakwani na Muheza United kufanikiwa kuingia fainali na Korogwe Worrias baada ya kuifunga kwa mabao 2, 0.

No comments:

Post a Comment