Polisi
wamemkamata kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Kizza Besigye, ambaye
ni mgombea wa urais nchini Uganda, siku moja baada ya uchaguzi
kufanyika.
Kizza
Besigye aliwekwa kizuizini wakati polisi walipovamia Makao Makuu ya
chama chake, katika mji mkuu wa Kampala. Besigye alikuwa akitaka
kuitisha mkutano na waandishi wa habari. Mabomu ya machozi yamelipuliwa
nje ya jengo la makao makuu ya chama hicho.
Matokeo
rasmi ya uchaguzi kwa karibu nusu ya vituo vya kupigia kura
yametangazwa, Rais Yoweri Museveni anaongoza. Museveni anawania kwa
awamu ya tano, baada ya miaka 30 madarakani.
Kwa mujibu wa wa matokeo ya awali yaliyotolewa na tume, Museveni anaongoza kwa 62% ya kura, wakati Besigye ana 33% ya kura.
Polisi
bado hawajatoa kauli juu ya sababu ya kukamatwa Besigye. Ikiwa hii ni
mara ya tatu katika muda wa wiki moja kwa Kiongozi huyo kuwekwa
kizuizini.
Upigaji
kura bado unafanyika katika baadhi ya maeneo ambayo vifaa vya kupigia
kura vilichelewa kuwasili kwenye vituo, ambapo vituo hivyo
havikufunguliwa kabisa siku ya Alhamisi.
SOURCE: BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment