Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za
uchimbaji katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha
kwa kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo
hayo ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa
inaweza kuhatarisha uhai wa maisha yao.
Katika kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali
ambayo ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka
yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa
inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani
waliendelea na shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha
Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na
yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa
kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba
kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.
Alisema kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa
la vifo linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na
kanuni .
Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias Kadabila
alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya mkuu wa
wilaya ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala ambapo alisema kuwa pia
iatawasaidia kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na uchimbaji
holela.
Aidha pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa
ushirikiano ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo
kwa muda wa mwezi mmoja .
Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao ambapo
walisema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji
huo ndiyo ambao unawafanya kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto
na kwamba serikali iangalie namna nyingine.
"kwakweli tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi
wananachi ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia
tunaweza kula ,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha
maisha yetu"Alisema Lowayani Metili
Ipo haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na
serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati
wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga
wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.
No comments:
Post a Comment